TTCL

EQUITY

Tuesday, November 26, 2013

MWILI WA MWANACHUO JERRY MRUMA ALIYENYONGWA NCHINI KENYA WAWASILI DAR, KUZIKWA LEO MAKABURI YA KINONDONI



Baadhi ya wanafamilia, ndugu, jamaa na marafiki wa familia ya Isaack Mruma wakiwa wamebeba sanduku lililohifadhi mwili wa marehemu Jerry Isaack Mruma katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius NyerereJerry Mruma alifariki hivi karibuni jijini Nairobi, Kenya kwa kunyongwa na watu wasiojulikana na ni mtoto wa Mhariri Mtendaji wa zamani wa Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN), Isaack Mruma.
 
 
Marehemu Jerry Isaack Mruma enzi za uhai wake.

 
 Watoto wa Isaack Mruma, Kelvin Mruma (kulia) na kaka’ke Khan Mruma wakipeana faraja pamoja na mwanafamilia mwenzao wakati wakisubiri mwili wa ndugu yao.
 
Baadhi ya wanafamilia wakati wa kupokea mwili wa mpendwa wao.
 
 Wafanyakazi mbalimbali wa Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN) wakiwa uwanjani hapo.
 
 Kaimu Mhariri Mtendani wa TSN, Gabriel Nderumaki (kulia) akizungumza jambo na Mkurugenzi wa Mwananchi Comunication, Tido Mhando Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Dar es Salaam leo wakati wa kuupokea mwili wa Jerry Mruma mtoto wa Mhariri Mtendaji wa zamani wa TSN.
 
 Kaimu Mhariri Mtendaji wa Magazeti ya Serikali (TSN) ambako Isaack Mruma alikuwa akifanya kazi kama Mhariri Mtendaji, Gabriel Nderumaki (kulia) akimfariji Mruma kufuatia msiba wa kijana wake Jerry Mruma akliyefariki kwa kuuwa nchini Kenya.
 
 Mkurugenzi wa Mwananchi Communication, Tido Mhando akimfariji Isaack Mruma.
 
Isaack Mruma akifarijiwa na mmoja wa watoto wake Kelvin Mruma uwanjani hapo mara baada ya kuupokea mwili wa Jerry.
 
Mhariri wa Gazeti la Habarileo, Joseph Kulangwa (kulia) akimfariji Isaack Mruma kutokana na msiba huo wa mwanaye.
 
Mwili wa Mwanachuo Jerry Mruma aliyefariki kwa kunyongwa na watu wasiojulikana nchini Kenya umewasili nchini jana na ndege ya Shirika la Kenya Airways na unatarajiwa kuzikwa leo mchana makaburi ya Kinondoni jijini Dar baada ya ibada itakayofanyika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Usharika wa Mbezi Beach, Dar.

No comments:

Post a Comment