TTCL

EQUITY

Wednesday, October 9, 2013

HII NDIO TAFSIRI HALISI YA AMANI, UTULIVU NA UPENDO WA TANZANIA


Wimbo wetu wa Taifa unaanza na Mungu Ibariki Afrika kabla ya Mungu Ibariki Tanzania katika ubeti wa pili. Hii iliwekwa kwa kusudio. Afrika ilitangulia kwanza. Wakati Raila Odinga aliponyimwa nyaraka za kusafiri na serikali ya kikoloni ya Kenya, nchi yetu ilimpa pasi ya kusafiria, ya nchi yetu. Mifano kama hii ipo mingi kuonyesha utayari wa siku zote wa Tanzania kutanguliza mbele ushirikiano na umoja na nchi nyingine za Afrika. Wakati taifa lilipokuwa katika matatizo makubwa ya kiuchumi miaka ya 1970 bado nchi yetu ilitoa fedha kusaidia wapiganaji wa ukombozi Zimbabwe na Msumbiji. Mojawapo ya mkutano muhimu katika historia ya chama cha ANC cha Afrika Kusini wa kuamua mwelekeo mpya wa mapambano ya uhuru wa kutumia silaha pia ulifanyika hapa Tanzania, Morogoro mwaka 1969, kadi ya chama cha FRELIMO ya mpigania uhuru wa Msumbiji, hayati Samora Machel alipewa kwa mara ya kwanza akiwa Dar es Salaam, tarehe 22 Februari 1965. Mwalimu Julius Nyerera alikuwa tayari kuahirisha uhuru wa nchi yetu ili kusubiri Kenya na Uganda, tupate uhuru siku moja na kutangaza nchi moja ya Afrika Mashariki siku hiyo. Suala la msingi ni kwamba kizazi cha vijana wa sasa Afrika kina jukumu na nafasi ya kuifanya Afrika kuwa moja.Wimbo wetu wa Taifa unaanza na Mungu Ibariki Afrika kabla ya Mungu Ibariki Tanzania katika ubeti wa pili. Hii iliwekwa kwa kusudio. Afrika ilitangulia kwanza. Wakati Raila Odinga aliponyimwa nyaraka za kusafiri na serikali ya kikoloni ya Kenya, nchi yetu ilimpa pasi ya kusafiria, ya nchi yetu. Mifano kama hii ipo mingi kuonyesha utayari wa siku zote wa Tanzania kutanguliza mbele ushirikiano na umoja na nchi nyingine za Afrika. Wakati taifa lilipokuwa katika matatizo makubwa ya kiuchumi miaka ya 1970 bado nchi yetu ilitoa fedha kusaidia wapiganaji wa ukombozi Zimbabwe na Msumbiji. Mojawapo ya mkutano muhimu katika historia ya chama cha ANC cha Afrika Kusini wa kuamua mwelekeo mpya wa mapambano ya uhuru wa kutumia silaha pia ulifanyika hapa Tanzania, Morogoro mwaka 1969, kadi ya chama cha FRELIMO ya mpigania uhuru wa Msumbiji, hayati Samora Machel alipewa kwa mara ya kwanza akiwa Dar es Salaam, tarehe 22 Februari 1965. Mwalimu Julius Nyerera alikuwa tayari kuahirisha uhuru wa nchi yetu ili kusubiri Kenya na Uganda, tupate uhuru siku moja na kutangaza nchi moja ya Afrika Mashariki siku hiyo. Suala la msingi ni kwamba kizazi cha vijana wa sasa Afrika kina jukumu na nafasi ya kuifanya Afrika kuwa moja.

No comments:

Post a Comment