TTCL

EQUITY

Thursday, February 18, 2016

Prof. Mbarawa azishukia Temesa, TTCL.

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa.
 
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, ameelezea kutoridhishwa kwake na utendaji      kazi  wa  Wakala wa Umeme na Ufundi (Temesa) juu ya uendeshaji wa vivuko na ukusanyaji mapato.
 
Sambamba na hilo, ameitaka Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) kubadilika kiutendaji ili kujiendesha kibiashara badala ya kutegemea serikali.  
 
Akizungumza jana na wafanyakazi wa wizara hiyo mjini hapa, Profesa Mbarawa, alisema serikali itachukua uamuzi mgumu ikiwamo kuwachukulia hatua wale wanaoshindwa kuwajibika. 
 
Alisema wizara ilitangaza kutumia Sh. bilioni 60 kufanya matengenezo na ukarabati mkubwa wa uwanja wa ndege wa Musoma ili kuwaondolea adha wananchi wa mkoa na watalii wanaofika kutembelea hifadhi ya taifa ya Serengeti.
 
Alisema   hatua  hiyo  inalenga    kumuenzi   Baba    wa  Taifa  Hayati  Mwalimu Julius Nyerere, hivyo  serikali  imetenga  dola   milioni  30 (zaidi ya  Sh. bilioni 60 kwa ajili ya kazi hiyo.
 
Aliongeza ulegevu katika kazi umesababisha  adha kubwa  kwa   wananchi  ambao   sasa   wanalazimika kusafiri   hadi   mkoani   Mwanza  kutafuta huduma  hiyo  huku   uwanja  huo  ukikosa mapato. 
 
Kuhusu   Kampuni  ya Simu  Tanzania (TTCL), Profesa Mbarawa alisema inapaswa kubadilika kiutendaji badala ya kutegemea serikali kufanya biashara ili kuongeza pato la taifa. 
 
Hivi karibuni, Profesa Mbarawa alianza kazi ya kusafisha taasisi Zilizo chini ya wizara yake kwa kuwang’oa vigogo waandamizi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (THA) na kuwahamishia makao makuu ya wizara. Pia alimsimamisha kazi meneja wa Fedha wa Kampuni ya Ndege Tanzania (ATCL) kwa ubadhirifu wa mamilioni ya fedha.  

No comments:

Post a Comment