Mtwara,Tanzania
WAKATI Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Jakaya Kikwete na
Serikali yake ikihaha kutafuta mbinu za kuzima vurugu za Wananchi wa
Mtwara wanaopinga hatua ya Serikali hiyo kusafirisha gesi kwa njia ya
mabomba kutoka Mtwara hadi jijini Dar es Salaam,watu wawili wameripotiwa
kuuwawa jioni hii.
Taarifa zilizonaswa na Habarimpya.com kutoka Mtwara
zinadai kwamba vurugu hizo zinaendelea katika baadhi ya maeno ya
Magomeni na maeneo ya Sokoni kiasi cha kusababisha vifo vya watu wawili.
Kati ya watu waliofariki Dunia katika vurugu hizo leo ni pamoja na
Mama Mjamzito anayedaiwa kupigwa risasi wakati wa mambano ya Askari wa
Jeshi la Polisi na wananchi hao. mwingine aliyedaiwa kupigwa risasi
katika vurugu hizo leo ni mwanafunzi wa Chuno huku mwingine akikimbizwa
katika Hospitali ya Ligula kwa matibabu zaidi.
Mbali na mauaji hayo ya raia wasiokuwa na hatia, wananchi wa eneo la
Magomeni Mkoani hapo pia wanadaiwa kukimbilia katika Hospitali hiyo ya
Mkoa kuomba hifadhi wakihofia usalama wao kutokana na vurugu za kuchomwa
kwa nyumba zao pamoja na vibanda vya biashara zilizotokea leo asubuhi
katika eneo hilo.
"Ingawa katika baadhi ya mitaa hali
imetulia na ni idadi ndogo ya wananchi ndiyo inayoonekana wakitembea
mitaani isipokua eneo la Magomeni ambako mabomu yanaendelea kusikika
huku huduma za kijamii katika mji huo zikiwa zimesimama zikiwemo
usafiri, huduma za kibenki na shule"alisema Ramadhani Omary Mkazi wa
Magomeni Mtwara.
No comments:
Post a Comment