Asema vurugu za Mtwara zinatokana na njaa
Dar es Salaam
WAKATI Serikali ikiendelea kuwatupia wanasiasa lawama kuhusiana
na vurugu za wakazi wa Mtwara wanaopinga hatua ya Rais Kikwete na
Serikali kusafirisha Gesi hadi jijini Dar es Salaam kwa njia ya mabomba,
Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Dk Willbroad Slaa, amesema kwamba machafuko yanayotokea katika mkoa huo hayasababishwi na mambo ya kisiasa isipokuwa ni umaskini unaoikabili nchi.
Dk Slaa alisema kwamba umaskini huo unaosababisha vurugu za
Mtwara zimesababishwa na CCM tangu zama za kale na si kwa siasa za
sasa. “Yanayotokea Mtwara ni
matokeo ya umaskini ambao CCM imewaletea wananchi. Mtwara wanakumbuka ya
Mwadui, Geita na North Mara. Wanayakataa”alisema Dk Slaa katika Ukurasa
wake wa Tweeter.
Alisema kwamba Wananchi hao
wameamua kufanya yote hayo kwa kuangalia wenzao wa mikoa mingine
iliyojaliwa kuwa na mali nyingi katika mikoa yao na bado haiwanufaishi
matokeo yake inakuwa ni mali yakuwanufaisha wengine bila wao kupata
faida yoyote ile.
Katika hatua nyingine Dk Slaa
alisema kwamba Serikali isikimbilie kulaumu wanasiasa bali itambue
kwamba,siasa chafu zinafanya kazi kama watu ni masikini, lakini kama
nchi itakuwa tajiri siasa chafu haziwezi kuwepo.
No comments:
Post a Comment