Membe atuhumiwa vurugu za Mtwara
Dar es Salaam
WAKATI vurugu za Wananchi wa Mtwara zikiendelea na kusababisha
vifo vya watu wawili akiwemo Mama mjamzito, huku Askari wanne wakifariki
Dunia katika ajali ya gari walipokuwa wakitokea Nachingwea kuelekea
Mtwara kutuliza vurugu hizo, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikano wa
Kimataifa Bernard Membe anatuhumiwa kuhusika katika vurugu hizo.
Waziri Membe anakuwa mtu watatu
kuhusishwa na vurugu hizo ikiwa ni siku chache baada ya Mbunge wa Kigoma
Kaskazini, Naibu Katibu Mkuu wa Chadema na Naibu Kiongozi wa kambi ya
Upinzani Bungeni, Zitto Kabwe kutupiwa lawama kedekede kwamba ndiye
mfadhili mkuu wa vurugu za Mtwara.
Hata hivyo tuhuma hizo za Zitto
ziliyeyuka baada ya watu mbalimbali waliotoa tuhuma hizo kukosa
ushahidi, huku serikali pia ikikosa ushahidi wa kumtia Mbunge huyo wa
Chadema hatiani kutokana na vurugu hizo.
Wakati watu wakiendelea kutafakari
juu ya tuhuma hizo, Mwenyekiti wa Chama Cha Wananchi (CUF) Profesa
Haruna Ibrahim Lipumba naye akarushiwa lawama kama hizo kwamba ndiye
mchochezi mkubwa wa ruvugu za Mtwara.
Leo hii Waziri Membe ametupiwa
lawama hizo kutoka kwa wabunge wa CCM ambao walisema kwamba Waziri Membe
ndiye chanzo cha vurugu hizo na kufanya idadi ya wanasiasa
waliotuhumiwa kuhusika katika tukio hilo kufika watatu.
Tuhuma za kwamba Membe anakabwa koo na wabunge wa CCM kwamba anahusika katika vurugu za Mtwara zilinaswa na Habarimpya.com kutoka vyanzo vya habari ndani ya CCM.
Mbali na Habarimpya.com
kudokezwa juu ya tuhuma hizo za Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano
wa Kimataifa Bernard Membe, Mbunge wa Kigoma Kaskazini pia alianika
tuhuma hizo katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Tweeter. Akichati
na watu mbalimbali akiwemo @Carol Ndosi, aliyemwambia Zitto kwamba,
"Kwa maoni yangu, bomba sio tatizo la msingi. Bomba Ni alama ya
kuwaunganisha tu wananchi"alisema Carol Ndosi alipokuwa akichati na
Zitto.
"Badala ya kutafuta suluhisho la
kudumu, Mtwara tunatafutana. Rais analaumu wanasiasa. Waziri Nchimbi
analaumu wanasiasa. Kweli? Ndio chanzo? Hatuishi
vituko sisi, sasa wabunge wa CCM wanasema Waziri wa Mambo ya Nje ndio
anachochea vurugu Mtwara. Ilikuwa Zitto, kisha Lipumba...."alisema Zitto
Katika Ukurasa wake wa Tweeter.
No comments:
Post a Comment