Siku
moja baada ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) kugoma
kwa kukosa mikopo ya kuwakimu kimaisha, Rais Dk. John Pombe Magufuli
amewambia wanafunzi wa chuo hicho kuwa anaelewa changamoto zinzowakabili
wanafunzi hao.
Dk.
Magufuli alisema hayo wakati alipokuwa akifanya uzinduzi wa jiwe la
msingi la ujenzi wa maktaba ya kisasa ambayo itajengwa chuoni hapo kwa
udhamini wa serikali ya China wenye thamani wa Dola Milioni 41.2.
Rais
Magufuli alisema kuwa serikali ya awamu ya tano imejipanga kuyafanyia
kazi matatizo yaliyopo chuoni hapo na kuwaahidi wanafunzi wa chuo hicho
kikubwa nchini kuwa hatawaangusha atahakikisha matatizo yaliyopo chuoni
hapo yanatafutiwa usumbufu.
“Chuo
hiki kina historia kubwa Afrika na hata duniani, shida ambazo
zinawapata wanafunzi wa UDSM hata mimi nimeziishi niwambie tu jambo moja
kuwa sitawaangusha,” alisema Dk. Magufuli.
Aidha
Rais Magufuli ameimwagia sifa serikali ya China kwa ufadhili huo
nakuitaja kama moja ya nchi iliyo na urafiki wa kweli na Tanzania lakini
pia kumpongeza Rais wa awamu ya nne na Mkuu wa Chuo cha UDSM, Dk.
Jakaya Kikwete kwa kuomba ufadhili huo akiwa madarakani na sasa matokeo
yake yanaonekana kuwa mazuri.
Kwa
upande wa Mkuu wa Chuo hicho ambaye ni Rais wa Awamu ya Nne, Dk. Jakaya
Kikwete alisema chuo hicho kina changamoto nyingi zikiwepo miondombinu
na upatikanaji wa maji safi na hivyo kumuomba Rais Magufuli kuangalia
jinsi anavyoweza kumaliza changamoto hiyo.
“Wakati
sisi tunaingia tulikuwa 350 ila kwa sasa wanafika hadi 7,000 kwa mwaka
kwahiyo nikuombe uangalie ni jinsi gani utatusaidia kumaliza changamoto
hizi, ulinipa kazi na mimi nimeifanya kama ulivyoniagiza,
“Changamoto
ni nyingi na hata ukiangalia asilimia 30 pekee ya wanafunzi wa chuo
ndiyo wanapata nafasi katika hosteli za chuo wengine asilimia 70 wanajua
wenyewe wanapoishi na kama unavyofahamu wengi wanatoka maeneo ya mbali
inakuwa ni changamoto kubwa kwao,” alisema Dk. Kikwete.
No comments:
Post a Comment