Uchunguzi kuhusiana na mauaji ya kutisha yaliyojaa utata unaendelea kufuatia kuuawa kwa watu wanane mkoani Tanga Tanzania.
Mauaji hayo yamekuja wiki chache kufuatia mengine yaliyotokea katika mikoa ya Dar es Salaam, Mwanza na Pwani.
Kuhusiana
na mauaji ya Tanga, Kamanda wa polisi mkoani humo Leonard Paulo amesema
watu wanaohofiwa kuwa ni majambazi waliwateka wakaazi wa Kitongoji cha
Mabatini wilayani Tanga kutoka majumbani kwao na kuwaua kwa kuwakata
kata na mapanga.
Mauaji hayo yalifanyika karibu na eneo ambalo
liko jirani na Mapango ya Amboni, ambapo Februari mwaka jana kulitokea
mapigano yaliyosababisha vifo ikiwemo askari polisi mmoja.
Habari zinasema wauaji katika tukio hilo la Tanga walijitambulisga kama.
Akisimulia
maauaji hayo yalivyotokea mke wa mmoja ya waliouawa alisema wakatio
wakiwa wamelala waligongewa na watu wasiojulikana ambao walijitambulisha
kama askari na kumnchukua mume wake na kumtaka wampeleke kwa kaka yake
ambaye pia walimuuuapamoha na watu wengine.
No comments:
Post a Comment