TTCL

EQUITY

Friday, May 27, 2016

Wafanyabiashara wa simu waomba kuongezwa muda wa kuzimwa kwa simu feki.

Wakati juni 16 mwaka huu simu zote feki zikitarajiwa kuzimwa baadhi ya wafanyabiashara za simu za mikononi katika jijini Dar es Salaam, na baadhi ya mikoa walalamikia kukosa kabisa wateja na kupata hasara kubwa kutokana na kuwa na simu nyingi ambazo ni feki huku watuamiaji nao wakilalamikia kuwa watakosa mawasiliano kutokana na simu origino kuwa ghali.
S.erikali imesisitiza kuwa haitaongeza muda wa kuzifungia simu feki kwani inataka Watanzania wajifunze kufuata taratibu. Aidha, imesema itatoa muongozo wa namna ya kuzitupa simu hizo kwa kuwa ni taka maalumu ambazo hazitakiwi kutupwa hovyo.
Hayo yalisemwa jana Dar es Salaam na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa wakati wa uzinduzi wa nembo mpya ya Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) na huduma ya 4G LTE.
Profesa Mbarawa alisema kuwa ufungiaji huo unalenga kuhakikisha kuwa simu na vifaa vyote vya mawasiliano vinavyotumika nchini, vinakuwa halisi vyenye ubora na vinavyokidhi sifa za huduma.
Aliwataka wananchi kuzingatia kikamilifu maelekezo yanayotolewa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kuhusu namna ya kuzitambua simu feki. Akizungumzia uzinduzi wa nembo hiyo, Profesa Mbarawa alisema kuwa serikali itaiwezesha TTCL kwa kuiongezea masafa ya megahezi 800 waweze kuingia katika soko la ushindani la mawasiliano nchini.
Alisema awali waliipa TTCL megahezi 1800 ambazo zimesaidia kuingia katika mtandao wa kasi wa 4G LTE kwamba kampuni hiyo pekee haiwezi kununua masafa hayo. Ofisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Dk Kamugisha Kazaura alisema kuwa wameboresha miundombinu ya simu za mezani na mkononi kwa kuleta teknolojia ya 2G GSM, 3G UMTS na LTE sokoni kwenda sambamba na ushindani
Baadhi ya watumiaji waliozungumza na mwandishi wetu nao wameitupia lawama serikali kwa kutoa agizo la kuzimwa kwa simu feki huku ikiruhusu simu hizo kuingia nchini na kuzitaka mamlaka husika kulitizama upya swala hilo ama kuweka bei elekezi kwa simu halisi ili iwe rahisi kwa wananchi wa kipato cha chini kuzinunua.
Wapo baadhi ya wauzaji wa simu pia walioipongeza serikali kwa hatua iliyochukuwa ya kuzima simu feki na walikuwa na haya ya kusema.
Mamlaka ya mawasiliano nchini TCRA tayari imeonesha msimamo na kutangaza kuwa juni 16, mwaka huu simu zote feki zitazimwa "Ikumbukwe kuwa zoezi la kufungiwa kwa simu feki sio geni kwa nchi za Afrika Mashariki ikiwemo Kenya ambao tayari wameshazifungia kabisa simu feki" alisema Dkt. Ally Yahaya Simba Mkurugenzi Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA).

No comments:

Post a Comment