Misri imesema kuwa
itachunguza madai kwamba mmoja wa maafisa wake aliwaita Waafrika
wanaoishi katika jangwa la sahara kuwa ''mbwa na watumwa'' wakati wa
mkutano jijini Nairobi.
Madai hayo yametajwa na mwanadiplomasia wa
Kenya ambaye anasema Misri inafaa kuzuiliwa kuwakilisha Afrika katika
majadiliano yoyote.
Lakini Cairo imesema kuwa hakuna ishara kwamba lugha kama hiyo ilitumika na kutaka ushahidi wowote uliorekodiwa kutolewa.
Kisa hicho huenda kikazua wasiwasi kati ya Msri na majirani zake wa Jangwa la Sahara.
Katika
malalamishi rasmi,Yvonne Khamati ,mwenyekiti wa kamati ya kiufundi ya
wanadiplomasia wa Afrika amesema kuwa kuwa matamshi hayo yalitolewa na
kiongozi wa ujumbe wa Misri katika mkutano wa Umoja wa Mataifa wiki
iliopita.
''Kulikuwa na mgawanyiko katika mkutano huo baada ya
makubaliano ya Gaza kutoidhinishwa kutokana na ukosefu wa
wanachama'',alisema Khamati.
''Matamshi hayo yaliotolewa kwa lugha ya Kiarabu yalitolewa katika mazungmzo na ujumbe wa Misri'',aliongezea Bi Khamati.
No comments:
Post a Comment