Katibu
Mkuu Kiongozi Dkt. John Kijazi ameutaka uongozi wa hospitali ya
Mwananyamala kuhakikisha kuwa dawati la malalamiko kwa wagonjwa
linafanya kazi masaa 24 ili kuboresha huduma katika hospitali hiyo.
Akizungumza
katika hafla ya kupokea msaada wa magodoro Dkt. Kijazi amesema kuwa
wagonjwa wanatakiwa kuhudumiwa kwa wakati na kusikilizwa malalamiko yao
muda wote wanapopatwa na changamoto hospitalini hapo ili kuweza
kuboresha huduma kwa watanzania.
“Nimepata
malalamiko kutoka kwa wananchi ambao walipata matatizo usiku wa kuamkia
leo na hakukuwa na mtu wa kuwasikiliza kwa wakati na kushindwa kupata
huduma bora walipokuwa na shida hivyo naagiza uongozi kuhakikisha dawati
la malalamiko kufanya kazi masaa 24 ili kuondoa kero za Wagonjwa
wote”.alisema Dkt Kijazi.
Aidha
Dkt. Kijazi ameushukuru uongozi wa Umoja wa Makanisa ya Pentekoste kwa
kutoa msaada wa magodoro 50 yenye thamani ya shilingi milioni 1.631 ili
kuendeleza huduma bora kwa wagonjwa wa Hospitali ya Mwananyamala jijini
Dar es salaam.
Mkuu
wa Wilaya ya Kinondoni Bw. Ally Hapi wa kwanza kushoto akimsikiliza
mmoja wa wagonjwa wanaotibiwa katika hospitali ya Mwananyamala akitoa
kero zake kuhusu hospitali hiyo wakati wa hafla fupi ya kupokea msaada
wa magodoro 50 kutoka kwa Umoja wa Makanisa ya pentekoste iliyofanyika
katika hospitalini hapo.
Akipokea
msaada huo Dkt. Kijazi alisema kuwa anawaomba viongozi wa Umoja huo na
taasisi zingineziendelee na moyo wa kuchangia kwenye shughuli za
kijamii kadriwanavyoweza ili kuifikisha Tanzania salama katika kilele
cha mafanikio.
“Nawaomba
Umoja wenu, taasisi na wadhamini mbalimbali kuweza kusaidia kuinua na
kukuza huduma bora za kijamii ikiwemo mahospitalini ili kusaidia
serikali kupiga hatua katika kupambana na changamoto ya vifaa
zinazoikabili hospitali ya Mwananyamala” aliongeza Dkt. Kijazi.
Kwa
upande wa Mkuu wa wilaya ya Kinondoni Bw. Ally Hapi amesema kuwa ana
Imani na Serikali ya awamu ya tano katika kutatua kero za wananchi
hususani katika Wilaya yake kwani ameshaona mfano wa kupokea msaada huo
na kuungwa mkono na Katibu Mkuu Dkt. John Kijazi kwa kushirikiana vizuri
kwenye shughuli hiyo.
“Nafurahi
kukutana na kushirikiana kwa pamoja na Katibu Mkuu Kiongozi katika
shughuli za kijamii hususani katika hili la kuendeleza huduma bora
zitolewazo na hospitali ya Mwananyamala ili kuifikisha mbali Tanzania
mpya” alisema Bw. Hapi.
No comments:
Post a Comment