Mkurugenzi Mtendaji Tume ya Kudhibiti Ukimwi Bibi. Fatma Mrisho (kushoto) akiteta jambo na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, na Walemavu Dkt. Abdallah Possi wakati wa shirikisho la vijana na wadau wa vijana kuhusu masuala ya VVU na UKIMWI.
Serikali imedhamiria kuhakikisha kuwa vijana wote nchini wanashirikishwa kikamilifu na kupatiwa huduma zinazotakiwa ili kumaliza uwepo wa maambukizi mapya ya virusi vya ukimwi, kupunguza ubaguzi na unyanyapaa unaotokana na ukimwi pamoja na kupunguza vifo vitokanavyo na ukimwi kwa vijana.
Hayo yamesemwa na Naibu
Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na
Walemavu Dkt. Abdallah Possi alipokua akifungua mkutano wa mwaka wa wadau wa
masuala ya vijana leo Jijini Dar es Salaam.
Dkt.
Possi amesema kuwa asilimia 2 ya maambukizi mapya ya virusi vya ukimwi yapo
miongoni mwa vijana wenye umri kati ya miaka 15 hadi 24 ambapo ushamiri kwa
vijana wa kike uko juu zaidi ya ule wa vijana wa kiume hasa katika umri wa
miaka 23 hadi 24.
Baadhi ya
vijana na wadau wa vijana akifuatilia kwa makini mada zilizokua
zikiendelea wakati wa mkutano wa mwaka wa wadau wa masuala ya vijana.
Akizungumza wakati wa mkutano huo Mkurugenzi Mtendaji Tume ya kudhibiti Ukimwi Bibi. Fatma Mrisho amesema kuwa Tume inaendelea kushirikiana na jamii kuhakikisha kuwa watoto na vijana wanapata kinga na huduma stahiki kupunguza utegemezi hivyo kuwafanya vijana kujiamini na kujitokeza kupambana na VVU/UKIMWI
Akizungumza wakati wa mkutano huo Mkurugenzi Mtendaji Tume ya kudhibiti Ukimwi Bibi. Fatma Mrisho amesema kuwa Tume inaendelea kushirikiana na jamii kuhakikisha kuwa watoto na vijana wanapata kinga na huduma stahiki kupunguza utegemezi hivyo kuwafanya vijana kujiamini na kujitokeza kupambana na VVU/UKIMWI
“Vijana
ni nguvu kazi ya taifa la leo, wakipatiwa nafasi ya kujitambua na kuwasilisha
hisia zao utegemezi ndani yao utapungua, ni vyema vijana wakaandaliwa mazingira
ambayo watakua huru kushiriki katika masuala ya VVU na UKIMWI” Alisema Bibi.
Mrisho.
Aidha
Bibi. Mshiro amemtaka kila kijana aliyeshiriki mkutano huo kubeba mambo muhimu manne
na kuwafikishia vijana wengine kumi waliopo vijiweni, maofisini ama sehemu
nyingine yeyote ile ili kuweza kusambaza elimu waliyoipata kwa kila kijana nchi
nzima na kuokoa afya za vijana wenzao.
Kwa upande wake
kijana anayeishi kwa matumaini Bi. Wittiness Nakanje ameiomba serikali
kuanzisha kliniki maalumu za vijana wanaoishi na VVU/UKIMWI ili kuwaweka vijana
kuwa huru kujitokeza kwa wingi kupima afya zao na kupata elimu ya VVU na UKIMWI.
Kulingana
na utafiti wa viashiria vya UKIMWI kwa mwaka 2011/2012 tanzania inajumla ya vijana
milioni 12 wa umri wa 10 hadi 19 ikiwa ni asilimia 24 na milioni 16 wa umri wa
miaka 19 hadi 24 ikiwa ni asilimia 24 ya Watanzania wapatao milioni 44, idadi
hiyo ya vijana inajumuisha wasichana wapatao 7,430,840 na wavulana 6,924,612.
Kwa
mujibu wa Sensa ya watu na makazi ya mwaka 2012 vijana wa umri wa miaka 19 hadi
24 wako 3, 954,039 ambapo wasichana
idadi yao ni 2,160,986 sawa na asilimia 55 na wavulana 1,793,053 sawa na
asilimia 45.
No comments:
Post a Comment