Mkurugenzi Upimaji na Ramani wa Wizara ya
Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Bw. Justo Lyamuya akionesha ramani
sahihi ya Tanzania leo jijini Dar es Salaam. kulia ni Mkurugenzi
Msaidizi Mipaka ya Kimataifa wa Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya
Makazi Dkt. James Mtamakaya.
WIZARA ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya
Makazi imebaini kuwepo kwa ongezeko la matumizi ya ramani ya Tanzania
ambayo mipaka yake imepotoshwa, Upotoshwaji huu umefanywa kwenye “diary”
(vitabu vya kumbukumbu na matukio), Kalenda, mabango, matangazo ya
kwenye vyombo vya habari na sehemu nyinginezo. Jambo hilo la kupotosha
mipaka ni hatari kwa usalama wa nchi.
Ramani sahihi ya Tanzania inatakiwa
kuonesha mpaka kwa sehemu ya maziwa ya Victoria, Tanganyika na Nyasa
ukipita katikati ya maziwa hayo. Hivi karibuni tumebaini matumizi ya
ramani yaTanzania kwenye majarida, magazeti na hata Luninga
inayopotosha mpaka kwa sehemu ya ziwa Nyasa ikionesha mpaka kupita
pembezoni mwa ziwa.
Kitendo cha kuchapisha ramani yenye
makosa kwa kutumiavyanzo visivyo rasmi ni kosa kwa mujibu wa mamlaka
(Instrument) ya Mhe. Waziri aliyepewa dhamana ya kusimamia sekta ya
ardhi ikiwemo masuala ya upimaji na ramani.
Idara ya Upimaji na Ramani ambayo ndiyo
yenye mamlaka ya kuandaa, kuchapisha, kutunza na kusambaza ramani zote
nchini ipo tayari kutoa ramani kwa matumizi yaliyokusudiwa ikiwa ni
pamoja na kutoa elimu na ushauri kuhusu usahihi wa ramani kabla ya
kuitumia.
No comments:
Post a Comment