SERIKALI
kupitia wakala ya Serikali mtandao imesema kuwa inaendelea kulifanyia
kazi suala la uanzishaji wa mfumo wa TEHAMA utakaowawezesha wananchi
kupata huduma na taarifa mbalimbali za Serikali kupitia simu zao mkononi
mahali popote walipo kwa njia ya mtandao.
Utaratibu
huo pia utawawezesha wahitimu wa vyuo mbalimbali vya elimu nchini
Tanzania kupata taarifa za ajira za Serikali na kuwawezesha kuomba
nafasi hizo, kufuatilia majibu ya usaili walioufanya na kupata taarifa za kuitwa kazini kupitia namba za utambulisho watakazopewa kupitia ujumbe mfupi (sms).
Akizungumza
na Wahariri wa vyombo vya Habari leo jijini Dar es salaam Mtendaji Mkuu
wa Wakala ya Serikali Mtandao (e-Government Agency) Dkt. Jabiri Bakari
amesema kuwa mfumo huo
utamuwezesha mwananchi kupata huduma za Serikali mahali popote alipo
kufuatia mifumo ya TEHAMA kuwasiliana na kubadilishana taarifa.
Amesema kuwa dhana ya Serikali Mtandao ni
kuwa na matumizi ya TEHAMA kwenye shughuli zote za Serikali kwa lengo
la kuongeza ufanisi na kupunguza gharama za uendeshaji kwenye huduma za
Afya, Utalii, Malipo ya tozo za huduma,vibali, leseni ,elimu na huduma
mbalimbali za Serikali.
Dkt. Jabiri amesema moja
ya vitu vinavyosababisha usumbufu kwa wananchi kutokana na kukosekana
kwa Serikali mtandao ni pale wanapohitaji kupata huduma za Serikali
ikiwemo Hati ya kusafiria ambapo hulazimika kwenda Idara ya Uhamiaji
kujaza fomu maalum na kisha kusubiri kwa muda wa zaidi ya wiki moja ili
taarifa zao ziweze kuhakikiwa na taasisi nyingine za Serikali wakati
suala hilo lingeweza kuchukua siku moja.
“Matumizi ya TEHAMA kwenye shughuli za Serikali hurahisiaha sana upatikanaji wa taarifa kwa
kuwa mifumo inawasiliana na kubadilishana taarifa haimlazimu mwananchi
kwenda kwenye taasisi zaidi ya tano kupata huduma yake” Amesisitiza Dkt.
Jabiri.
Amesema
taasisi za Serikali kama Jeshi la Polisi, Mamlaka ya Vitambulisho vya
Taifa (NIDA), Idara ya Uhamiaji, RITA na taasisi nyingine ambazo
majukumu yao hutegemeana kupitia serikali mtandaomifumo ya taasisi hizo
huunganishwa ili ifanye kazi pamoja kwa lengo la kuruhusu mifumo
kuzungumza kumuhudumia mwanachi bila yeye kulazimia kuzifuata taasisi hizo.
Amesema kuwa pamoja na maboresho mbalimbali yanayoendelea ndani ya Serikali ya kujenga Serikali mtandao imara mfumo uliopo sasa kwenye baadhi ya taasisi humfanya mwananchi achukue muda mrefu kupata huduma.
Ameeleza
kuwa taasisi za Serikali zinazofanya kazi katika mazingira yanayofanana
zinaposhirikiana katika kutoa huduma Kupitia Serikali mtandao mwananchi
wa kawaida hatajua nini kinaendelea, atakachokipata mwisho ni majibu ya
huduma aliyoiomba kama ni Bandarini atachukua
mzigo bila usumbufu wowote kwa kuwa suala la kodi, upakuaji na upakiaji
wa mizigo na ukaguzi halitamgusa mwananchi.
Ameongeza
kuwa ili Serikali mtandao iweze kufanya kazi yake ipasavyo nchini
lazima kuwe na miundombinu ndani ya taasisi au nje pia uwepo wa mifumo
Tumizi ( Application Systems) inayoshughulikia masuala mbalimbali,
wafanyakazi pamoja na Sera, miongozo na taratibu za kusimamia TEHAMA kuwezesha huduma mtandao ( e - Servieces).
Msemaji wa
Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Bi Mboza Luandiko
akifafanua kwa waandishi wa Habari (hawapo pichani) kuhusu namna mfumo
mpya wa kupokea habari na taarifa mbalimbali kwa njia ya simu ya kiganjani.
Dkt. Jabiri amesisitiza Tanzania iko kwenye hatua ya kwanza na ya pili, kwa maana ya taasisi nyingi za Serikali zina tovuti zenye taarifa za awali za kumsaidia mtu kujua nini kinapatikana au kutolewa na taasisi za serikali ili aweze kuchukua hatua ya kupata huduma.
Dkt. Jabiri amesisitiza Tanzania iko kwenye hatua ya kwanza na ya pili, kwa maana ya taasisi nyingi za Serikali zina tovuti zenye taarifa za awali za kumsaidia mtu kujua nini kinapatikana au kutolewa na taasisi za serikali ili aweze kuchukua hatua ya kupata huduma.
Amesema
Wakala ya Serikali mtandao imefanikiwa kuweka mifumo kwa maana ya
Tovuti kuu ya Serikali, Tovuti ya Wananchi, Tovuti ya data huria ambayo
ina taarifa mbalimbali za wananchi kuhusu Maji, Barua pepe ya Serikali
(GMS) ambayo sasa inatumiwa na jumla ya taasisi 117 za Serikali na
Balozi mbalimbali kwa lengo kuepuka matumizi ya barua pepe za muda.
Amebainisha
kuwa Wakala ya Serikali Mtandao kwa sasa eGA katika awamu ya kwanza
imeziuganisha taasisi 75 za serikali na Wizara zote za Serikali kupitia
mkongo wa taifa, pia Wakala imeziunganisha Taasisi 72 zilizounganishwa
kwa simu zinazotumia itifaki ya Intaneti kwenye mkongo wa taifa ili
kurahisisha mawasiliano na kupunguza gharama.
Akijibu
Suala la baadhi ya Taasisi za serikali kukawia kuunganishwa kwenye
mtandao amesema kuwa awali hakukuwa na mfumo huo kutokana na baadhi ya
mapungufu yaliyojitokeza kwenye Sera, miongozo na taratibu zinazosimamia
utendaji wa shughuli za kila siku serikali lakini sasa kuna mwongozo wa
taasisi kuzingatia ili kuhakikisha mifumo ya taasisi za Serikali
inawasiliana ili kufanya kazi pamoja kuondoa mapungufu yaliyokuwepo.
Aidha,
mifumo ya utendaji kazi inabadilika kulingana na mabadiliko yanayotokea
kwenye taasisi hizo na kuongeza kuwa Wakala ya Serikali mtandao imekuwa
makini sana kuhakikisha hakuna mfumo unaoinuka dhidi ya mwingine lengo
likiwa kumhakikishia mwananchi kupata huduma katika eneo moja kwa muda
mfupi.
Kwa
upande wake Meneja Habari,Elimu na Mawasiliano wa Wakala hiyo Bi. Suzan
Mshakangoto amesema kuwa suala la matumizi ya mitandao mbalimbali isiyo
rasmi katika shughuli za serikali linafanyiwa kazi huku akisisitiza
kwamba utaratibu unaandali wa kuhakikisha kuwa mawasiliano yote ya
matumizi ya barua pepe nje ya zile za serikali kwenye ofisi za umma
yanafungwa kuanzia Saa 1:30 hadi saa 9:30.
Kwa
sasa ni taasisi 72 tu za serikali zikiwemo Wizara zote, Wakala, Bunge
na taasisi zimeunganishw, Aidha halmashauri 77 zimeunganishwa na mkongo
wa taifa na kazi ya kuzifikia taasisi zote 500 inaendelea ili kuwezesha
zoezi la kufunga huduma za mawasiliano za serikali nje ya mkongo wa
taifa.
Takribani
taasisi 200 za umma zina tovuti ili kurahisisha upatikanaji wataarifa
na huduma kwa wananchi. Changamoto iliyopo ni Tovuti nyingi kukosa
taarifa zilizohuishwa pia kuunganisha maeneo ambayo bado hayajafikiwa
hasa Halmashsuri na vijiji ili kuwezesha taarifa mbalimbali kupatikana
kwa wakati.
Wakala
imepata mafanikio katika utekelezaji wa jitihada za Serikali mtandao
hasa katika uwekaji wa mifumo ya Serikali kwa maana ya Tovuti kuu ya
Serikali, Tovuti ya Wananchi, Tovuti ya data huria ambayo ina taarifa
mbalimbali za wananchi kuhusu Maji, Barua pepe za Serikali ambayo sasa
ina taasisi 117 na Balozi mbalimbali zinatumia GMS ili kuepuka matumizi
ya barua pepe za muda.
Wakala
ya Serikali Mtandao katika awamu ya kwanza imeunganisha taasisi 72 za
serikali na Wizara zote za Serikali kupitia mkongo wa taifa pia
imeziunganisha taasisi hizo na simu zinazotumia itifaki ya intaneti
kwenye mkongo wa taifa ili kurahisisha mawasiliano na kupunguza gharama.
Akifafanua
kuhusu hatua ya mifumo ya serikali kuchelewa kufanya kazi pamoja
amesema hapo awali hakukuwa na mfumo uliowezesha jambo hilo kufanyika
kutokana na baadhi ya mapungufu yaliyojitokeza
kwenye Sera, miongozo na taratibu zinazosimamia masuala ya TEHAMA nchini
lakini sasa kuna mwongozo uliotolewa kuhakikisha mifumo ya taasisi za
Serikali inawasiliana na kufanya kazi pamoja ili kuondoa mapungufu yaliyokuwepo.
Aidha,
mifumo ya utendaji kazi inabadilika kulingana na mabadiliko yanayotokea
kwenye taasisi hizo na kuongeza kuwa Wakala ya Serikali mtandao imekuwa
makini sana kuhakikisha hakuna mfumo unaoinuka dhidi ya mwingine lengo
likiwa kumhakikishia mwananchi kupata huduma katika eneo moja kwa muda
mfupi.
Meneja
Habari, Mawasiliano Suzan Mshekangoto amesema suala la matumizi ya
mitandao mbalimbali isiyo rasmi katika shughuli za serikali linafanyiwa
kazi huku akisisitiza kwamba utaratibu unaandaliwa kuhakikisha kuwa
mawasiliano yote ya matumizi ya barua pepe nje ya zile za serikali
kwenye ofisi za umma yanafungwa kuanzia Saa 1:30 hadi saa 9:30 alasiri.
Amefafanua
kuwa taasisi 72 za serikali zikiwemo Wizara zote, Wakala, Bunge na
Mahakama zimeunganishwa, Aidha halmashauri 77 zimeunganishwa na mkongo
wa taifa na kazi ya kuzifikia zilizobaki inaendelea ili kuwezesha
mawasiliano ya serikali kupita kwenye mkongo wa taifa.
Bi.
Suzan amesema mpaka sasa takribani taasisi 200 za umma zina tovuti
zenye taarifa za huduma mbalimbali zinazotolewa na Serikali huku Changamoto iliyopo ni baadhi ya Tovuti hizo kukosa taarifa zilizohuishwa.
No comments:
Post a Comment