Serikali
kupitia Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi inaandaa Mpango
Kabambe wa Mipango Miji (Master Plan) utakaoainisha matumizi bora ya
ardhi na kuondoa migogoro ya ardhi nchini.
Kauli
hiyo ilitolewa Bungeni Mjini Dodoma na Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba
na Maendeleo ya Makazi Mhe. Angelina Mabula wakati akijibu maswali ya
wabunge kuhusu mpango wa Serikali kumaliza migogoro ya ardhi kwenye
maeneo mbalimbali nchini.
Mhe.
Mabula alieleza kuwa Wizara yake inashirikiana na Halmashauri za
Wilaya na Miji 18 kwenye program ya Urban Local Government Supporting
Programme (ULGSP) katika kuandaa Mipango Miji hiyo.
Pia
Mhe. Mabula alibainisha kuwa Wizara inaandaa na kukamilisha programu ya
kupanga, kupima na kumilikisha kila kipande cha ardhi Tanzania
itakayotekelezwa kwa kipindi cha miaka kumi kuanzia 2015 hadi 2025.
“Serikali
imekuwa ikiziagiza Halmashauri kutenga fedha kwa ajili ya ununuzi wa
vifaa vya upimaji kwa kuwa inatambua umuhimu wa kupima viwanja na
mashamba ili kuwa na matumizi bora ya ardhi yetu” alisema Mabula.
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Angelina Mabula
Aidha,
Mabula aliongeza kuwa Serikali kupitia Mradi wa Benki ya Dunia ipo
katika mchakato wa kununua vifaa vya upimaji ambavyo vitasambazwa katika
kanda 8 za Wizara ya Ardhi ili Halmashauri zote zilizopo ndani ya kanda
hizo ziweze kunufaika.
Alieleza
kuwa makadirio ya awali ya gharama za mradi huo ni Dola za Kimarekani
Milioni 4 ambapo Dola Milioni 2 zitatumika kwenye upimaji na Dola
Milioni 2 zitatumika kwa ajili ya ununuzi wa Vifaa.
Katika
kupunguza na kutatua migogoro ya ardhi iliyopo sasa, Mabula alisema
kuwa Wizara ya Ardhi imeandaa kitabu cha orodha ya migogoro nchi nzima
kinachoainisha vyanzo vya migogoro hiyo ili hatua stahiki ziweze
kuchukuliwa.
Hali
kadhalika, Mabula alisema kuwa Wizara imesambaza Sera na Sheria za
Ardhi hasa kwenye maeneo yenye migogoro, wameimairisha mfumo wa
kielektroniki katika kutunza kumbukumbu, na kuboresha ofisi za Kanda
ili kusogeza huduma za ardhi karibu na wananchi.
No comments:
Post a Comment