Serikali
ya Tanzania kupitia Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo
zimekubaliana kubadilishana uzoefu na mafunzo katika masuala ya filamu,
haki miliki na Sera.
Hayo
yamesemwa na Waziri wa Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape
Nnauye alipokuwa akiongea na balozi wa afrika kusini nchini ofisini
kwake jijini dar es Salaam.
Waziri
nape amemwomba balozi uyo nafasi hiyo kwa sababu afrika kusini ipo
vizuri zaidi na mbali katika sekta ya filamu na kwayo itakuwa nafasi
nzuri kwa nchi izi mbili kukaa pamoja ili wabadilishane uzoefu na hasa
suala la haki miliki na sera,kwani serikali yetu iko mbioni kutengeneza
sera madhubuti ili sekta hii ya filamu iwe rasmi.
Alieleza
kuwa ili tusonge mbele hatuna budi kuangalia kwa wenzetu wanafanyaje
ili litatuongezea ujuzi na maarifa wakati tunajipanga na mengine kwani
wageni sasa wameanza kuingia Tanzania kwa kuwa inafanya vizuri katika
sekta hii ya filamu na ivyo ni wajibu wetu kuhakikisha tunatengeneza
sera na mazingira madhubuti ili wakija wasiondoke.
Waziri
wa Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape Nnauye akifurahi jambo
na Balozi wa Afrika kusini nchini Tanzania Bw.Thamsanga Mseleku
alipomtembelea ofisini kwake jijini Dar es Salaam.Katika maongezi yao
wamekubaliana kushirikiana katika masuala ya sekta ya filamu na hasa
katika kubadilishana uzoefu katika mambo ya haki miliki na Sera.
Kwa
upande wake Balozi wa Afrika kusini nchini Tanzania Bw. Thamsanga
Mseleku ameishukuru serikali yake kuendelea kuimarisha mahusiano baina
yao na amehaidi kufanikisha makubaliano ya kukutanisha wasanii kutoka
afrika kusini na wa Tanzania ili wabadilishane uzoefu ili watoe kazi
zenye viwango bora Zaidi ili kazi zao zifike mbali.
Makubaliano
haya yamekuja baada ya wasanii wa filamu Single Mtambalike na Elizabeth
Michael kushinda Tuzo katika Africa magic Viewer’s choice Awards na
walipomtembelea ofisini kwake walimwomba waziri uyo mwenye dhamana
kuwasaidia kutengeneza Sera madhubuti ili sekta hii iwe rasmi na
wanufaike na jasho lao.
Balozi
wa Afrika kusini nchini Tanzania Bw.Thamsanga Mseleku akisaini kitabu
cha wageni wakati alipomtembelea Waziri wa Habari, Utamaduni,Sanaa na
Michezo Mhe.Nape Nnauye ofisini kwake jijini dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment