TTCL

EQUITY

Monday, March 14, 2016

MWENYEKITI WA SERIKALI YA MTAA ATOA MSAADA WA VIFAA VYA KUSOMEA, KATIKA SHULE YAKE

Mh. Godfrey Mushi mwenyekiti Mtaa wa Themi Mashariki (wa katikati, mwenye koti la suti) akizungumza na mmoja wa wagane wake walotembelea shule ya mtaa wake na kutoa msaada wa kompyuta.
Mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa Themi mashariki Mh. Godfrey Mushi, mwishoni mwa wiki iliyopita kwakushirikiana na marafiki zake kutoka marekani wametoa msaada wa kompyu pakato (Laptop), vifaa vya kufundishia elimu ya awali, vifaa vya michezo, vitabu, madaftari na kalamu kwa uongozi wa shule ya msingi engira iliyopo katika mtaa wake.
Mh. Mwenyekiti katikati akiwa na Mkuu wa shule mara baada ya kukabidhiwa kompyuta na wageni.
Wageni wakiandaa zawadi zao, tayari kwa kugawa
Mh. Mushi kwa kushirikiana na marafiki zake wa marekani amesema kuwa wametoa msaada huo kama njia mojawapo ya kuunga mkono juhudi nzuri za kitaaluma zinazofanywa na uongozi wa shule, ambapo alisema "Shule imekuwa ikijitahidi sana, pamoja na kuwepo kwa changamoto nyingi lakini bado ufaulu umekuwa ni wakuridhisha tofauti na ilivyo kwa kata na mitaa mingine" akizungmza hayo alitolea mfano shule ya sekondari iliyopo korona iliyoshika nafasi ya mwisho na ikihesabika katika kundi la shule 10 za mwisho.

Mkuu wa shule ya Engira Bwa. Backari kwa niaba ya waalimu na uongozi wa shule alitoa shukrani zake za dhati kwa Mh. Mwenyekiti, "tunashukuru sana, na tunakuombea kheri. kwa msaada huu, naamini tutapiga hatua zaidi" alisema.

Aidha Mkuu wa shule aliongeza kusema kuwa shule inampongeza sana Mh. Mwenyekiti kwa juhudi na ushirikiano wake wa dhati katika kuhakikisha  misingi ya elimu inaimarika katika mtaa wake, ambapo amekuwa akifuatilia kwa karibu maendeleo ya shule, na taaluma ya wanafunzi. "Jambo kama hili ni la kuigwa na kiongozi yeyote na wa ngazi yoyote, hii kwangu ni fahari kubwa kuwa na kiongozi mtendaji na mwajibikaji kama huyu. Na matunda yake tumeanza kula, na tunaahidi mavuno mengi zaidi" alimalizia kusema.
Mh. Mwenyekiti akitoa nasaha kwa wanafunzi na uongozi wa shule.
Mwenyekiti aliuomba uongozi wa shule kuwa na ushirikiano mzuri wa kitaaluma, nakusema kuwa "Serikali ya mtaa kwa kushirikiana na bodi ya shule, Mh. Diwani na wazazi tunafanya mkakati wa pamoja katika kuhakikisha upatikanaji wa chakula kwa wanafunzi wawapo shule unawezekana. Hii ni kwasababu tunataka Shule ya Msingi Engira kuwa mfano mzuri wa kuigwa na wengine kimaendeleo na kitaaluma kwa ujumla, hilo ni la msingi zaidi. Mimi nawatakia utumishi mwema" alisema.

Vilevile alitoa ushauri na kusema "Pamoja na kwamba bodi ya shule ni mpya, lakini ikishirikiana vyema na waalimu pamoja na wazazi na wakatambua wajibu wao, na kupeana ushirikano mzuri kwa pamoja watafanikiwa kudhibiti suala la utoro, na kusaidia kiwango cha elimu kupanda" alimalizia kusema kuwa serikali inapaswa kuhakikisha inatatua kero za waalimu, iwape mahitaji yao ya msingi na kuwalipa mishahara yao kwa wakati hii itachangia morali kwa waalimu kuwa na bidii ya ufundishaji.

Picha ya pamoja wageni, waalimu na Mh. Mwenyekiti

No comments:

Post a Comment