Mamlaka
ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (UWERA) imesema kuwa imepokea
maombi kutoka Shirika la Umeme nchini ili kupunguza gharama za umeme
nchini.
Akizungumza
na waandishi wa habari, Mkurugenzi Mkuu wa EWURA, Felix Ngamlagosi na
kueleza kuwa Februari, 24 UWERA ilipokea maombi kutoka TANESCO ambayo
inaelezea mabadiliko ya bei ya umeme kwa miaka miwili kuanzia April, 1.
Mkurugenzi Mkuu wa EWURA, Felix Ngamlagosi akizungumza na waandishi wa habari.
“TANESCO
wamewasilisha ombi husika kulingana na kifungu NA. 24(2) cha Sheria ya
Umeme Naa. 131 kinachoitaka mamlaka kufanya mabadiliko ya bei
zinazotozwa kwa mtoa huduma mara moja kila baada ya miaka mitatu,
“Pendekezo
la wastani wa badiliko la umeme ni asilimia 1.1 kuanzia Aprili, 1 mwaka
huu na asilimia 7.9 kuanzia Januari, 1, 2017,” alisema Ngamlagosi.
Alisema
kuwa mujibu wa kifungu Na. 19(2) (b) cha sheria za EWURA, sura NA. 414
wanatakiwa kuanzisha mchakato wa kupata maoni ya wadau ili kujua uhalali
wa maombi ya mapendekezo ya bei za huduma iliyoyapokea kutoka TANESCO.
Aliongeza kuwa mkutano wa kukusanya maoni kutoka kwa wadau utafanyika Machi, 4 jijini Sa res Salaam.
No comments:
Post a Comment