Mratibu
wa shirika la Riksfobundent For Sexual Upplysning,Jonas Lillberg
(kushoto) na kulia ni Jenny Fors kutoka shirika la WaterAid
Sweden,wakizingua mnara wa tanki la maji katika zahanati ya kijiji cha
Mwankoko manispaa ya Singida lilojengwa na SEMA kwa ufadhili kutoka
WaterAid Tanzania na RFSU.
Watendaji
wa serikali ngazi mbali mbali ambao vituo vya afya na hospitali
vimenufaika na ukarabati mkubwa wa majengo na uboreshaji wa miundo mbinu
ya maji wametakiwa wafanye juhudi za ziada kuwahamasisha akina mama
wajawazito kujifungulia kwenye vituo hivyo vya afya kwa ajili ya
usalama wao na watoto wao wachanga.
Imedaiwa
kuwa vituo hivyo vya afya, zahanati, hospitali ya rufaa mjini hapa na
hospitali ya wilaya ya Iramba, miundo mbinu yake ikiwemo ya maji na
ukarabati wa majengo umechangia akina mama wajawazito na wananchi
kukimbia matibabu katika maeneo hayo.
Mratibu
wa shirika la Riksfobundent For Sexual Upplysning,Jonas Lillberg,akitoa
nasaha zake mbele ya mkutano wa wadau wa sekta ya afya,muda mfupi baada
ya kukagua utekelezaji wa mradi wa ‘mwanzo mwema’ unaofadhiliwa na
shirika la WaterAid likishirikiana na shirika la RFSU ya nchini
Sweden.Kushoto kwake ni afisa WaterAid Tanzania Cushbert Maendaenda na
kulia ni Jenny Fors kutoka WaterAid makao makuu Sweden.
Mratibu
wa Shirika la Kimataifa la Sweden Riksfobundent For Sexual Upplysing
(RFSU), Jonas Tillberg ametoa wito huo juzi muda mfupi baada ya kukagua
utekelezaji wa mradi wa ‘Wash’ uliokarabati zahanati na miundombinu ya
maji katika kijiji cha Mwankoko, uliofadhiliwa na WaterAid Tanzania na
RFSU Sweden na kutekelezwa na shirika la SEMA.
Alisema
kuwa baada ya yeye na timu yake kutoka nchini Sedwen kukagua miradi
wanayoifadhili wamefurahishwa na utekelezaji wake na sasa ombi lao ni
walengwa wa mradi kutumia fursa hiyo kikamilifu kwa ajili ya afya zao.
“Wananchi
wa Sweden na wafadhili wowote duniani hupenda na hufurahishwa wakiona
fedha walizotoa msaada zinawanufaisha walengwa kwa muda mrefu na si
vingenevyo,” alisema Tillberg.
Katika
hatua nyingine Meneja wa Shirika lisilo la kiserikali la Sustainable
Environment Management Action (SEMA), Ivo Manyaku alisema wanatarajia
kutumia zaidi ya shilingi 600 milioni kwa ajili ya kugharamia mradi wa
‘Wash’ ambao uboresha wa sekta ya afya na elimu katika wilaya ya Iramba
na Manispaa ya Singida.
Alisema
mradi huo unaendelea kufanya ukarabati mkubwa katika hospitali ya
wilaya ya Iramba na pia vituo viwili vya afya na baadhi ya shule za
msingi katika Wilaya ya Iramba pia kuweka miundombinu ya maji.
Baadhi
ya akina mama wakazi wa kijiji cha Mwankoko manispaa ya Singida,wakiwa
kliniki iliyopo kwenye zahanati ya kijiji kwa ajili ya watoto wao
wachanga kupimwa afya zao.Zaahanati ya Mwankoko ni moja ya vituo vya
afya vilivyonufaika na msaada wa zaidi ya shilingi 600 milioni
zilizotumika kuboresha miundo mbinu ya maji na ukarabati wa majengo.
“Manispaa
ya Singida vile vile itanufaika na mradi huo kwa kuboreshewa hospital
ya rufaa, kituo cha afya cha Sokoine, zahanati ya kijiji cha Mwankoko na
baadhi ya shule,” alisema.
Ivo alisema lengo la mradi huo ni
pamoja na kumaliza tatizo la uhaba wa maji kwenye vituo vya afya na
hospitali linalochangia maradhi yanayosababisha vifo kwa akina mama
wajawazito na watoto wachanga.
Aidha Ivo alisema chini ya
mradi huo wanatoa mafunzo kwa baadhi ya watumishi wa idara ya afya
yanayohusu usafi wa mazingira, usafi binafsi na utunzaji na namna bora
ya matumizi ya miundombinu mbalimbali.
Kwa upande wake Mganga Mkuu wa
Wilaya ya Iramba, Dkt. Boniface Richard aliwashukru wafadhili wa
WaterAid na RFSU kwa kufadhili wa ukarabati mkubwa na uboreshaji wa
miundo mbinu ya maji safi na salama kwa hospitali ya wilaya na baadhi ya
vituo vya afya.
“Serikali kuu kupitia Wizara
yake ya afya imekuwa ikifanya juhudi kubwa kuhakikisha hospitali, vituo
vya afya na zahanati zinakuwa na vifaa tiba na madawa lakini suala la
maji limekuwa halipewi kipaumbele,” alisema.
Mkurugenzi
wa mipango shirika la WaterAid Tanzania,Abel Dugange,akizungumza kwenye
mkutano wa hadhara katika kijiji cha Mgongo tarafa ya Shelui wilaya ya
Iramba,ambao uliitishwa kwa ajili ya wananchi kupewa ujumbe wa afya ya
uzazi na umuhimu wa wananume kushiriki.
Akifafanua
Dkt.Richard alisema kabla ya mradi huu unaotekelezwa vema na SEMA,
hospitali, vituo vya afya ni zahanati, vilikuwa vinakabiliwa na uhaba
mkubwa wa maji.
Akifafanua
zaidi amedai kuwa kutokana na uhaba huo wagonjwa walilazimika kuleta
maji machafu kutoka kwenye madimbwi kitendo kilichokuwa ni hatari zaidi
kwa afya zao.
“Maji safi na salama ni muhimu
sana kwa ajili ya usafi wa mazingira, usafi binafsi na usafi wa vifaa
tiba. Maji yakiwepo ya kutosha kwenye hospitali na vituo vya afya
itasaidia sana kupunguza magonjwa yanayosababisha vifo vya akina mama
wajawazito na watoto wao wachanga. Niwahakikishie tu ndugu zetu
wafadhili kuwa miundombinu hii ya maji iliyoboreshwa na ukarabati wa
majengo, tutaitunza na kuilinda kikamilifu,” alisema Mganga huyo Mkuu wa
Wilaya.
Meneja
wa shirika la SEMA,Ivo Manyaku (wa kwanza kulia) akiwa amepumzika na
wafadhili kutoka WaterAid Sweden na wananchi wa kijiji cha Mwankoko nje
ya zahanati ya kijiji hicho juzi.Picha na Nathaniel Limu.
Baadhi
ya wafadhali wa mradi wa ‘Mwanzo Mwema’ na wananchi wa kijiji cha
Mgongo wilaya ya rmba, muda mfupi baada ya kuzinduliwa kwa mradi wa
ukarabati mkubwa na uboreshaji wa miundo mbinu ya maji uliofadhiliwa na
mashirika ya WaterAid Tanzania na RFSU na kutekelezwa kwa ufanisi na
shirika la SEMA.
No comments:
Post a Comment