Serikali
nchini UBELGIJI imefuta sherehe za kuukaribisha mwaka mpya katika mji
wa BRUSSELS kutokana na hofu ya kutokea kwa shambulio la kigaidi
UBELGIJI yafuta sherehe za mwaka mpya
Serikali nchini UBELGIJI imefuta sherehe za kuukaribisha
mwaka mpya katika mji wa BRUSSELS kutokana na hofu ya kutokea kwa
shambulio la kigaidi.
Uamuzi huo ulichukuliwa baada ya serikali ya nchi hiyo kupata taarifa
kuhusu njama za kutekeleza shambulio la kigaidi katika mji huo.
Meya wa BRUSSELS, YVAN MAYEUER, amesema sherehe hizo zinakusanya
zaidi ya watu laki moja mahali pamoja na hivyo ni vigumu kuwadhibiti
watu wote.
Hofu ya kutokea kwa shambulio la kigaidi katika sherehe za mkesha wa
mwaka mpya iliongezeka, baada ya polisi kukamata watu wawili kwa tuhuma
za kupanga mashambulio katika sherehe za mwaka mpya mjini BRUSSELS.
Mji huo wenye wakazi zaidi ya milioni 1 umekuwa katika hali ya
tahadhari tangu kutokea kwa mashambulio ya kigaidi mjini PARIS nchini
UFARANSA.
No comments:
Post a Comment