Waziri
wa Afya , Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu
jana alitembelea Makao Makuu ya Bohari ya Dawa (MSD) na kuahidi kuwa
balozi wa kuhakikisha deni la serikali linalipwa ili......... kuiwezesha MSD kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi.
Waziri
huyo alieleza hayo baada ya Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Laurean Bwanakunu
kueleza kuwa ukosefu wa fedha na deni la serikali ni changamoto kubwa
inayoathiri utekelezaji mzuri wa majukumu ya MSD.
Mbali
na hilo, Waziri wa Afya alisema mbali na deni hilo, hata kiasi cha
fedha kinachotengwa na serikali kwaajili ya hospitali, vituo vya afya na
zahanati na kununua dawa hakitoshelezi mahitaji, hivyo lazima suala
hilo lifanyiwe kazi mapema, huku akisisitiza hata kiasi hicho kidogo
kinachopatikana kitumike vizuri.
Katika
hatua nyingine aliishauri Bohari ya Dawa kuanza utaratibu wa kununua
dawa na vifaa tiba moja kwa moja kutoka kwa wazalishaji, kuhakikisha
dawa muhimu zinapatikana wakati wote na kuiagiza MSD itangaze kwenye
vyombo vya habari dawa zote ambazo zinapelekwa vituoni, zahanati na
kwenye hospitali, ambapo Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Laurean Bwanakunu
alieleza kuwa tayari MSD imeshaanza kubandika kwenye mbao za matangazo
za hospitali orodha ya dawa inazofikisha.
Waziri
huyo ambaye alifuatana na Katibu Mkuu wa Wizara, Dkt. Donald Mbando na
watendaji wengine pia alitembelea maghala ya kuhifadhia dawa ya MSD,
jengo la ofisi linalojengwa pamoja na kuwa na mkutano na menejimenti ya
MSD, ambapo pamoja na mambo mengine aliipongeza MSD kwa hatua iliyofikia
ya kuweka nembo ya GOT kwenye vidonge vyake ili kudhibiti upotevu wa
dawa za serikali pamoja na kuanzisha maduka ya dawa Muhimbili, na
mengine yanayotarajia kufunguliwa hivi karibuni mkoani Mbeya, Arusha na
Mwanza.
Waziri
Ummy Mwalimu alihitimisha kwa kusema kuwa ajenda yake kuu ni
upatikanaji wa dawa kwa wakati, kama rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Dkt. John Magufuli alivyoaainisha, hivyo MSD itekeleze
majukumu yake ipasavyo kwani mafanikio ya MSD ni mafanikio kwake pia.
No comments:
Post a Comment