Askari
na maofisa wa polisi mkoani MWANZA wametakiwa kuzingatia maadili ya
kazi,miongozo ya jeshi hilo pamoja na sheria za nchi ili kujenga taswira
nzuri ya jeshi hilo kwa jamii
kamanda wa polisi mkoa wa MWANZA CHARLES MKUMBO
Askari na maofisa wa polisi mkoani MWANZA wametakiwa
kuzingatia maadili ya kazi,miongozo ya jeshi hilo pamoja na sheria za
nchi ili kujenga taswira nzuri ya jeshi hilo kwa jamii.
Wito huo umetolewa na aliyekuwa kamanda wa polisi mkoa wa MWANZA
CHARLES MKUMBO wakati akimtambulisha kamanda mpya wa polisi wa mkoa huo
JUSTUS KAMUGISHA kwa maofisa,wakaguzi na askari polisi wa vyeo
mbalimbali.
Awali akimtambulisha kamanda KAMUGISHA,aliyekuwa kamanda wa polisi wa
mkoa wa MWANZA CHARLES MKUMBO amewataka askari na maafisa hao wa polisi
kutekeleza kwa vitendo kauli mbiu ya serikali ya awamu ya tano ya HAPA
KAZI TU.
Kamanda KAMUGISHA amehamia MWANZA akitokea mkoani SHINYANGA ambapo
kamanda MKUMBO akihamishiwa makao makuu ya polisi kwa ajili ya kuongoza
kamisheni ya intelijensia ya jinai nchini.
Katika hatua nyingine kamanda JUSTUS KAMUGISHA amekutana na waandishi
wa habari na kuwahakikishia wakazi wa MWANZA kuwa polisi imejipanga
kuhakikisha sikukuu ya mwaka mpya inasherekewa kwa amani na utulivu.
No comments:
Post a Comment