Mwalimu wa mchezo wa Karate Tanzania Sensei Willy
Ringo, amesema kuchelewa kufanyika uchaguzi wa viongozi wapya wa chama
cha karate Tanzania kunakwamisha juhudi zake za kueneza mchezo huo
mashuleni.
Mwalimu
wa mchezo wa Karate Tanzania Sensei Willy Ringo,amesema kuchelewa
kufanyika uchaguzi wa viongozi wapya wa chama cha karate Tanzania
kunakwamisha juhudi zake za kueneza mchezo huo mashuleni.
Ringo ambaye ana kituo cha mchezo wa shotokan-karate kwenye kituo cha
Utamaduni cha Urusi(Russian Culture Center) jijini Dar es
Salaam,amesema alikuwa mwenyekiti wa kamati ya kupeleka malalamiko
kwenye baraza la michezo Tanzania BMT, baada ya kuona muda wa viongozi
wa chama umemalizika.
Amesema bado kuna dana dana juu ya uchaguzi huo utafanyika lini,ila
mikatati yao kama wadau ni kuhakikisha mapema mwaka ujao chama cha
Karate kinafanya uchaguzi.
Aidha Ringo amesema pale chama cha Karate kitakaposimama ndiyo yeye
atakapoandaa programu ya kusambaza karate mashuleni,kwa kuwa atapata
baraka za chama na baraza la michezo na Wizara ya michezo.
No comments:
Post a Comment