MBUNGE
wa Ukonga, Mwita Waitara, amelazimika kusitisha mara moja ujenzi wa
uzio katika Shule ya Msingi Kivule Manispaa ya Ilala kutokana na eneo
hilo kuwa la shule.
Uzio huo ulikuwa ukijengwa na mtu asiyefahamika.
Hatua ya Waitara imekuja baada ya wazazi wa watoto wanasoma katika shule hiyo, kubaini eneo la shule likimegwa kinyemela.
Mbunge Waitara alifika katika eneo hilo na kukuta matofali yakiwa
yamerundikwa kisha akaamuru ujenzi wa uzio huo usitishwe mara moja.
“Naomba wananchi msivunje matofali hayo, nitafika Ofisi za Manispaa
ya Ilala na tutajua hilo eneo nani amelichukua na kuanza kufanya ujenzi
wakati akijua wazi ni mali ya shule na atakayebainika kuhusika na
uuzaji wa eneo hilo hatua kali dhidi yake zitachukuliwa,’’ alisema.
Mwenyekiti wa Kamati ya shule hiyo, Bihimba Nassoro, alisema hati
inaonysha kuwa eneo hilo ni la shule, lakini anashangaa kuona ujenzi
unafanyika eneo hilo na anayejenga bado hawajamfahamu.
Diwani wa kata ya Kivule, Moses Mollel, alisema eneo la shule lina
utata na kwamba haijulikani nani anajenga, hivyo ujenzi huo unapaswa
kusimamishwa ili kuondoa utata.
No comments:
Post a Comment