Rais
wa BURUNDI ametishia kupigana na kikosi cha Muungano wa Afrika cha
kulinda amani pindi wanajeshi hao watakapoingia nchini humo
Rais PIERRE NKURUNZIZA
Rais wa BURUNDI ametishia kupigana na kikosi cha Muungano wa
Afrika cha kulinda amani pindi wanajeshi hao watakapoingia nchini humo.
Akihutubia taifa kwa njia ya radio, rais PIERRE NKURUNZIZA amesema
kuingia kwa wanajeshi hao nchini BURUNDI kutakuwa ukiukaji wa uhuru wa
taifa hilo na pia shambulizi dhidi ya serikali yake.
Rais huyo alisusia ufunguzi wa mazungumzo ya amani nchini UGANDA siku ya Jumatatu.
NKURUNZINZA aliyeshinda muhula wa tatu katika uchaguzi mkuu
uliokumbwa na utata na maasi mwezi julai mwaka huu amekana kuwepo kwa
visa vya mauaji nchini mwake.
Viongozi wa kidini kutoka kanda ya Afrika Mashariki KENYA, TANZANIA,
RWANDA na UGANDA ambao wamekuwa wakikutana mjini NAIROBI ,wameelezea
wasiwasi wao na jinsi usalama unavyozidi kudorora katika taifa hilo.
No comments:
Post a Comment