WAFANYABIASHARA wakubwa wametajwa kuwa miongoni mwa watu fisadi zaidi sawa na maofisa wa polisi Barani Afrika.
Ni mara ya kwanza wafanyabiashara kutajwa kuwa mafisadi wakubwa
Barani Afrika na Shirika hilo limeongeza kuwa matumizi mabaya ya mamlaka
yanasababisha ongezeko la umaskini pamoja na kuwanyima raia mahitaji
muhimu.Hii ni kwa mujibu ya kura ya maoni iliyofanywa na shirika la kuchunguza ufisadi duniani la "Transparency International" ambalo limebainisha kuwa raia mmoja kati ya watano barani Afrika hutoa hongo.
Kwa mujibu wa Shirika hilo, watu wengi ambao ni maskini hujikuta mara kadhaa wakilazimika kulipa hongo ikilinganishwa na matajiri.
Nchi ya Liberia imetajwa kama inayoongoza kwa visa vya ufisadi Afrika huku ikifuatiwa na Cameroon, Nigeria na Sierra Leone.
Kwa upande wa Afrika Mashariki, Uganda inaongoza kwa visa vya ufisadi ikifuatiwa na Kenya huku Kusini mwa Afrika Zimbabwe na Zambia zikiongoza katika nchi zenye visa vingi vya ufisadi.
No comments:
Post a Comment