MAMLAKA ya Mapato
Tanzania (TRA) inaendelea Uchunguzi na ukaguzi kwenye makontena hayo
tisa yaliyokamatwa juzi, ambapo moja tayari limebainika kuwa na vifaa
vya ujenzi.
"Tuliyafungua juzi jioni na wamiliki wa makontena hayo walikuwepo,
moja ya makontena hayo lilikuwa na vifaa vya ujenzi hivyo kwa kuwa
hatutaki kuwaamini moja kwa moja kwamba kuna vifaa vya ujenzi pekee,
ndiyo sababu hivi sasa tunaendelea na kazi ya kupakua mzigo wote ili
kujiridhisha," alisema Kayombo.Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Mkurugenzi wa Elimu na Huduma kwa Mlipa Kodi wa TRA, Richard Kayombo, alisema Mamlaka hiyo ilianza kufungua makontena hayo juzi usiku kwa baadhi ya makontena.
Alisema makontena hayo ambayo ni mali ya Heritage Empire Company Ltd yenye namba ya mlipakodi (Tin) 116536501, bado wanaendelea kuyakagua kwa kutoa vifaa vyote vilivyomo ndani yake.
Aliongeza kuwa watakapokamilisha uhakiki wa kodi waliyolipa ndipo itatolewa taarifa kama ipo sawa au hapana.
No comments:
Post a Comment