Uchunguzi wa
shirika la habari la BBC umegundua kuwa kampuni ya kutengeneza sigara ya
British American Tobacco (BAT) imekuwa ikitoa hongo kwa wakuu
serikalini katika mataifa ya kanda ya Afrika Mashariki kwa nia ya
kuwashawishi kubadilisha sheria ilikulinda biashara ya tumbaku licha ya
madhara yake kwa afya ya wavutaji.
Ufichuzi huo umeibuka baada ya mfanyikazi mmoja kuipatia BBC stakabadhi zinazofichua ufisadi huo.BAT ilipoulizwa kuhusu ukweli wa madai hayo ya ufisadi iliiambia BBC kuwa
''Ukweli ni kuwa hatushiriki ufisadi kwa namna yeyote katika mataifa yeyote tunayohudumu''
Paul Hopkins, ambaye aliifanyia kazi kampuni hiyo ya BAT, nchini Kenya kwa miaka 13 anasema kuwa alianza kutoa hongo baada ya kuambiwa kuwa hiyo ni gharama ya kufanya biashara barani Afrika
"ukweli ni kwamba ikiwabidi kuvunja sheria ilikufaulu katika biashara huwa wanavunja sheria''
barua pepe zilizotumwa na Hopkins zinaonesha vipi mawasiliano yalianza na jinsi malipo yalivyotolewa.
Aidha Hopkins anaonesha jinsi BAT ilivyowapa hongo maafisa wa shirika la afya duniani WHO ambao wanasimamia udhibiti wa matumizi ya tumbaku ilikupunguza idadi ya watu wanaopoteza maisha yao kutokana na maradhi yanayotokana na matumizi ya mmea huo.
BURUNDI
Afisa mmoja wa FCTC nchini Burundi, Godefroid Kamwenubusa,na mwakilishi wa visiwa vya Comoros , Chaibou Bedja Abdou, walilipwa kiinua mgongo cha dola $3,000 (£2,000).
Wakati huohuo mwakilishi wa Rwanda, Bonaventure Nzeyimana, akatia kibindoni dola elfu $20,000.
Wote hao wamekanusha kupokea hongo kutoka kwa BAT.
RWANDA
Dakta Vera Da Costa e Silva, wa WHO, ameilaumu BAT na kusema kuwa "ni jambo la kufedhehesha sana''.
"hii ni unyama, kutumia fedha ilikupata faida huku maisha ya watu yakiangamia'' BAT sharti iadhibiwe vikali na serikali alisema bibi huyo.
BAT kimsingi iliwatumia watu waliopokea hongo kubadilisha sheria za nchi husika ilikuzuia biashara hiyo ya tumbaku isiathirike.
Kwa mfano wakala wa kampuni hiyo anasema katika moja ya nyaraka za siri kuwa Bwana Kamwenubusa atafuatilia na kufanikisha mabadiliko muhimu kabla rais wa nchi hiyo kutia sahihi na kuifanya kuwa sheria.
Comoros
Nchini Uingereza ni hatia kutoa hongo hata kama matukio hayo ya rushwa yalifanywa katika mataifa mengine.
BAT kwa upande wake inajitetea kwa kusema kuwa wafanyikazi wake walifanya makosa kinyume na maadili ya kampuni hiyo.
"Tunawahakikishia kuwa tunachunguza madai haya kwa nia ya kuadhibu wale watakaopatikana na hatia ya kukiuka maadili ya BAT''
''Wale wanaotoa madai hayo ni wafanyikazi wetu waliotimuliwa na hivyo tunahisi hizi ni njama za kulipiza kisasi''
Bwana Hopkins anasikika katika ukanda ulionaswa kisiri akimshauri wakili wa kampuni hiyo kuwa watu kadhaa watahitajika kulipwa ilikufunga vivywa vyao.
Wakili huyo Naushad Ramoly, anasikika akiuliza iwapo kuna watu wengine wanaostahili kulipwa ?''
Ramoly ambaye sasa hafanyikazi na BAT anasema kuwa hakushiriki ukiukaji wa maadili yeyote na wala hakuhusika katika shughuli zozote zinazokiuka sheria na kanuni''
Kenya
Mwaka wa 2012 afisa mmoja wa BAT , Adell-Owino anauliza fedha za kufanikisha safari ya waziri wa biashara wa Kenya Moses Wetangula.
Katika waraka huo Adell anasema kuwa waziri huyo Wetangula atalala katika jumba la ''Globe House" makao makuu ya BAT mjini London .
Adell-Owino anasisitiza kuwa hakutakuwa na stakabadhi zozote zinazoweza kuthibitisha malipo hayo.
BBC Panorama ilipomuuliza bwana Wetangula ambaye kwa sasa ni kiongozi wa upinzani nchini Kenya kuhusu ufichuzi huo, alisema kuwa ameshtushwa sana na madai hayo na akaonya kuwa atachukua hatua za kisheria dhidi ya mtu yeyote atakayeeneza habari hizo.
Wetangula alisema ''sikupokea pesa zozote wala tiketi ya ndege sijawahi kushirikiana na BAT."
Hata hivyo BAT iliwasilisha stakabadhi zinazoonesha kuwa malipo ya nauli ya ndege ilikuwa mojawepo ya njia za kutoa hongo kwa viongozi wakuu serikalini barani Afrika.
UGANDA
Nchini Uganda, mwanaharakati wa BAT Solomon Muyita aliyefutwa kazi mnamo mwaka wa 2013 alituhumiwa kwa kutoa hongo kwa watu 50 wakiwemo wabunge 7.
Muyita alisema kwa kinywa kipana kuwa yeye alikuwa akitekeleza maagizo ya kampuni hiyo ya BAT.
Kwa sasa amekwenda mahakamani akidai fidia kwa kufutwa kazi.
BAT inasema kuwa Muyita anasema uongo.
Akiwa mahakamani mwezi agosti 2015, Muyita alidai kuwa mbunge David Bahati, aliyekuwa akiwasilisha mswada wa kudhibiti matumizi ya tumbaku nchini Uganda alikuwa analipwa na kampuni ya BAT.
No comments:
Post a Comment