Akiwa
mmoja kati ya wanadada wanofanya vizuri sana kwenye Tasnia hii ya
BongoMovies ,Wema Sepetu ni msichana anayetoka kwenye Familia ya
kibalozi ni mtoto wa mwisho katika familia ya wasichana wanne wa Balozi
Isaack Sepetu Ibrahimu.
|
Alipata
elimu yake ya primary na sekondari katika shule ya ACADEMIC
INTERNATIONAL iliyopo jijini Dar es Salaam kabla ya kwenda Nchini
Malaysia kusomea mambo ya biashara za kimataifa katka chuo cha
Limkokwing University.
Wema alianza kuigiza rasmi mwaka 2007 alipoonekana kwenye filamu ya POINT OF NO RETURN ambapo halicheza kama mke wa jamaa tajiri mchawi ambaye daima huua wapenzi wake wa kike kama sadaka. Wema alifikiri angeweza kufa pia lakini aliamua kumwomba Mungu na mwishowe alifanikiwa kuiokoa familia yake na yeye.
Pamoja na filamu hizi Wema ameigiza kwenye filamu nyingine nyingi kama Red Valentine, White Maria, Tafrani, Sakata, Crazy Tenant, Diary, Lerato, Dj Benny and Basilisa zilizompatia umaarufu na mafanikio makubwa.
Pamoja na kuwa na kipaji cha uigizaji wema pia anakipaji kikubwa cha kuimba na pia alishawahi kushiriki mashindano ya urembo na kufanikiwa kutwaa taji la Miss Tanzania mnamo mwaka 2006 na kujipatia zawadi ya gari aina ya Toyota Rav 4.
No comments:
Post a Comment