MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA) mkoa wa Mwanza imeshindwa
kufikia lengo la ukusanyaji wa mapato katika kipindi cha mwaka 2013 –
2014, bila kubainishwa sababu za msingi zinazochangia ukusanyaji mdogo
wa mapato.
Hayo yaliibuka jana wakati wa ziara ya Mkuu huyo,
alipozungumza na wafanyakazi wa TRA namna ambavyo wanaendesha shughuli
zao za ukusanyaji wa mapato pamoja na changamoto zinazowakabili.
Meneja wa TRA Mkoa wa Mwanza, Elinsa Nyange, amesema TRA ilikusudia
kukusanya Sh. 4. 99 trilioni, katika kipindi cha mwaka 2013 lakini
ilikusanya Sh. 123 bilioni.
Pia amesema katika kipindi cha mwaka 2014, TRA ambayo inakusanya kodi
mikoa ya Mwanza na Geita iliweka lengo la kukusanya Sh 7.69 trilioni
lakini ilikusanya Sh. 123 bilioni, huku akishindwa kubainisha sababu za
msingi zinazosababisha kushindwa kukusanya kodi.
“Rais wa mkoa (Mkuu wa Mkoa wa Mwanza) nakuhakikishia tutaendelea
kuwaelimisha wananchi juu ya umhimu wa ukusanyaji wa kodi, pia mkoa wetu
na mikoa kama Arusha hailingani kwa vitega uchumi,” amesema Nyange.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Magesa Mulongo amesema sababu zinazotolewa na
meneja huyo hazina tija kwani ukusanyaji wa mapato kwa mkoa wa Arusha
upo juu ikilinganishwa na Mwanza.
Mulongo amesema kuwa mkoa wa Arusha katika kipindi cha mwaka 2013
ilikusanya Sh. 1.27 trilioni ikilinganishwa na Mwanza na Geita ambayo
inakusanya Sh. 123 bilion kitendo ambacho ni aibu kwa mikoa hiyo.
Hata hivyo amesema licha ya mkoa Mwanza kuwa ni moja kati ya mikoa
nchini yenye kiwango kikubwa cha uchumi ambao alidai unafikia trilioni
9, ukusanyaji wa mapato hafifu unachangiwa na watendaji wabovu.
“Serikali ya awamu ya tano inahitaji fedha na fedha zenyewe zinatoka
kwenu na inafahamu pesa zipo, kuweni makini katika ukusanyaji wa mapato
msikusanywe pesa kutoka kwa Wafanyabiashara wadogo kusanyeni na kwa
wakubwa,” amesema Mulongo.
No comments:
Post a Comment