December 1 hatua ya robo fainali ya michuano ya Kombe la Challenge 2015 iliendelea kwa timu ya taifa ya Rwanda ikiongozwa na mchezaji wa Dar Es Salaam Young African Haruna Niyonzima kucheza mchezo wao na timu ya taifa ya Kenya, ikiwa ni siku moja toka Kilimanjaro Stars itolewe na mwenyeji wa mashindano hayo Ethiopia kwa mikwaju ya penati.
December 1 imekuwa zamu ya timu ya taifa ya Kenya
kuaga michuano hiyo kwa mikwaju ya penati baada ya dakika 90 kumalizika
kwa sare 0-0, kwa mujibu wa sheria ya mashindano hayo dakika 90 za
michezo ya robo fainali ikimalizika bila kupata mshindi inapigwa mikwaju
ya penati kupata mshindi.
Rwanda wamefanikiwa kuibuka na ushindi wa jumla ya penati 5-3, mikwaju ya penati ya Haruna Niyonzima, Tuyisenge na Kizimana ilisaidia Rwanda
kutinga hatua ya robo fainli ya michuano hiyo, kwa matokeo hayo ni
rasmi Kenya ambao walikuwa mabingwa watetezi wa michuano hiyo wamevuliwa
ubingwa.
No comments:
Post a Comment