SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu nchini (TFF) linatarajia kufanya
mkutano wake Mkuu wa Mwaka kwenye Ukumbi wa Hoteli ya Regal Naivera
jijini Tanga ambapo wajumbe wa mkutano huo tayari walishatumiwa taarifa
za mkutano.
Akiongea na waandishi wa habari leo katika ukumbi
wa mikutano wa TFF, Kaimu Mkurugenzi wa Sheria na Wachama, Elliud Mvela
amesema maandalizi ya mkutano huo yanaendelea vizuri.
Mvella amesema ajenda za mkutano mkuu wa kawaida ni zile zilizopo
kikatiba, ila itaongezeka ajenda ya marekebisho ya katiba ambayo ni
mapendekezo yaliyotolewa na FIFA.
Agenda za mkutano mkuu ni:-
1.Kufungua Mkutano
2. Uhakiki wa Wajumbe
3. Kuthibitisha Ajenda.
4. Kuthibitisha Muhtsari wa Mkutano Mkuu uliopita.
5. Yatokanayo na Mkutano uliopita.
6. Hotuba ya Rais.
7. Ripoti kutoka kwa Wanachama
8. Kuthibitisha ripoti ya utekelezaji wa Kamati ya Utendaji.
9. Kuthibitisha ripoti ya Ukaguzi wa Hesabu 2013.
10. Kupitisha bajeti ya 2016
11. Marekebisho ya Katiba
12. Mengineyo
13. Kufunga Mkutano.
No comments:
Post a Comment