MAPATO
ya Serikali ya Tanzania yanayotokana na shughuli za uchimbaji
yameongezeka kwa asilimia 28 katika kipindi cha mwaka 2013/14, kwa
mujibu wa ripoti ya sita ya asasi nayoshughulika na biashara hiyo –
Tanzania Extractive Industries Transparency Initiative (TEITI) – kwa
kipindi kinachoishia Juni 30, mwaka jana.
Kwa
mujibu wa ripoti hiyo ambayo iliandaliwa na BDO East Africa na kutolewa
mjini Dar es Salaam na TEIT, licha ya kushuka kwa asilimia 10 kwa idadi
ya kampuni zinazohusika, mapato ya serikali kutokana na sekta ya
uchimbaji yaliongezeka kutoka Sh. bilioni 956 mwaka 2013 hadi kufikia
Sh. bilioni 1,221.
Ripoti
hiyo inasema ongezeko hilo kubwa lifikialo Sh. bilioni 265 linatokana
na ongezeko la uzalishaji wa dhahabu katika kipindi cha mwaka huo kwa
asilimia 10 hali kadhalika na malipo ya kodi ya taasisi yaliyofanywa na
Kampuni ya Ophir Tanzania (Block 1) ltd ya Sh. bilioni 361.
Ripoti
hiyo ya TEITI inalenga kusawazisha data iliyotolewa na kampuni hizo za
migodi na ile ya wizara na mashirika husika. Malengo ya jumla ya zoezi
hili la usawazishi ni kuisaidia serikali itambue mchango chanya
unaotolewa rasilimali za madini katika maendeleo ya kiuchumi na kijamii
ya nchi na kuelewa uwezo wake katika kuboresha usimamizi wa rasilimali
ili kujumuisha na kutekeleza kikamilifu misingi na vigezo vya TEITI.
Mwelekeo
wa stakabadhi za serikali kutokana na biashara ya uchumbaji katika
ripoti sita za EITI zilizochotwa kutoka katika ripoti za TEITI
zinaonesha kumekuwa na ongezeko la jumla ya mapato kwa asilimia 854
tangu kuwasilishwa kwa ripoti ya kwanza mwaka 2009. Ukijumlisha kampuni
zote za gesi na mafuta
Kumekuwa
na ongezeko la jumla la kampuni za gesi na migodi kutoka 11 mwaka 2009
hadi kufikia kampuni 59 mwaka 2014. Hata hivyo, ripoti hiyo inabainisha
kwamba kampuni zilizohakikiwa mwaka 2013 zilikuwa 65.
Kodi
ya taasisi iliyolipwa serikalini ilikuwa Sh. bilioni 492.490, ikiwa ni
asilimia 42.49 ya mapato yaliyokusanywa ambapo kodi ya mapato (PAYE) na
SDL zilichangia Sh. bilioni 162.885 ambazo ni sawa na asilimia 14.05 ya
mapato yote, kwa mujibu wa ripoti hiyo.
“Orodha
ya kampuni za uchimbaji zilizoteuliwa na shirika la Multi-Stakeholder
Group (MSG) kwa zoezi la usawazishi lilijumuisha kampuni 38 za uchimbaji
na 21 za mafuta na gesi na kufanya jumla ya kampuni kuwa 59. Karibu
kampuni zote zilizohusishwa katika zoezi hilo zimeshawasilisha taratibu
zao za kuripoti, isipokuwa nne.
Shughuli za uchimbaji wa madini anuai maeneo mbalimbali ya Tanzania.
Kampuni
nne ambazo zimesimaisha shughuli zao nchini Tanzania na ambazo hazipo
kabisa nchini hazikuwasilisha taratibu zao. Hata hivyo, jumla ya mapato
yaliyopokelewa na kutangazwa na taasisi za serikali kutoka kampuni hizo,
yalikuwa Sh. bilioni 2.5, ambayo ni sawa na asilimia 0.20 ya jumla ya
malipo yote yaliyofanyika serikalini.
Kampuni hizo nne ni Tanzanite One Trading Ltd., Songshan Geology Minerals Co. Ltd., Afren Gabon Ltd, na Siwandu Metal Ltd.
Ripoti
hiyo inasema kumekuwa na kuhitilafiana kuhusu malipo halisi kati ya
yale yaliyotajwa na kampuni za uchimbaji na yale yanayofahamika na
serikali mwanzoni mwa usuluhishi ambapo tofauti ilikuwa ya asilimia 1.69
ya mapato yote yaliyotangazwa na serikali.
Hata
hivyo, kwa mujibu wa ripoti hiyo, katika hitimishoo la usuluhishi,
tofauti halisi ikawa Sh. 2,428,572,571, ikiwa ni asilimia 0.20 ya jumla
ya malipo yote yaliyotangazwa na serikali
Ripoti
hiyo pia inasema kumekuwa na upungufu wa asilimia 10 katika ukusanyaji
mapato licha ya ongezeko la uzalishaji dhahabu kwa sababu ya kuporomoka
kwa bei ya dhahabu mwaka 2014. Jumla ya mapato yaliyoripotiwa na kampuni
hizo yalikuwa dola za Marekeni 2,146,062,181 mwaka 2014 ikilinganishwa
na dola 2,361,169,479 mwaka 2013.
Kwa
mujibu wa wastani wa bei ya dhahabu iliyokokotelewa kwa msingi wa
takwimu za kila mwezi, watani wa bei ya dhahabu ilipungua mwaka 2014
ikilinganishwa na mwaka 2013 kutokana na wastani wa dola 1,530.88 hadi
dola 1,264.99 kwa onzi ya trei, ambapo ni upungufu wa asilimia 17.
Wakati
upungufu wa mapato yatokanayo na madini unasababishwa zaidi na kushuka
kwa bei ya madini hayo mwaka 2014, kulikuwa pia na upungufu wa idadi ya
kampuni za migodi, kutoka kampuni 46 mwaka 2013 hadi kufikia 38 mwaka
2014 kwa sababu baadhi yao zilifunga shughuli zake nchini Tanzania.
Ophir
Tanzania (Block 1) Ltd ilifanya malipo ya jumla ya Sh.
361,938,833,000.00 (30%) kwa serikali ikiwa ya kwanza katika orodha ya
walipaji kumi bora wa kodi kwa mwaka 2014, ikifuatiwa na Geita Gold Mine
– Sh. 195,618,242,000 (16%), Bulyahulu Gold Mining Sh. 105,602,231,000
(9%), Pan African Energy Tanzania Ltd Sh. 76,907,992 (6%), na North Mara
Gold Mine Sh. 66,835,788 (5%).
Kampuni
nyingine katika orodha hiyo ya kampuni bora katika ulipaji kodi kwa
mwaka 2014 ni pamoja na Pangea Minerals Ltd., Songas Limited, Tanga
Cement Company Ltd, Tanzania Portland Cement Ltd., Statoil Tanzania AS
na Resolute Tanzania Ltd.
Tanzania
ilijiunga na TEITI mnamo Februari 2009 kufuatia mapendekezo yaliyokuwa
kama sehemu ya utekelezaji wa upembuzi yakinifu wa kuhakiki sekta ya
madini kwa mwaka 2007.
Kundi
la kazi la wadau – Multi-Stakeholder Working Group (MSG) – liliundwa
kusimamia utekelezaji wa EITI nchini Tanzania na liliwajumuisha
wawakilishi kutoka asasi za kijamii, kampuni za uchimbaji na serikali
yenyewe.
No comments:
Post a Comment