TTCL

EQUITY

Wednesday, December 9, 2015

Historia Fupi ya Halmashauri ya Jiji la Arusha


Neno Arusha linatokana na neno ARUSU (Kimasai) likiwa na maana ya eneo lenye majani mazuri ya malisho ambapo Ng’ombe aina ya RONOLARUSU (Ng’ombe wa rangi ya kijivu wenye madoadoa walilishiwa eneo hili).

Kutokana na uzuri wa eneo hili kimalisho kabila la wamasai na wameru waliweka makazi kwa sababu ya uhakika wa chakula cha mifugo yao.

Baada ya mji huu kuwa eneo maarufu la malisho idadi ya watu iliongezeka na shughuli mbalimbali haswa  za kibiashara zikaanza ambapo ziliweza kuvutia Wakoloni.

Wakoloni wa kwanza kuja Arusha ni wajerumani ambapo waliwatanguliza wamishionari lengo likiwa ni kutaka kutwaa eneo hili na kuwa makoloni yao.

 
Waarusha hawakukubali kutawaliwa kirahisi na waliweza kupigana na wamishenari hao na kuwaua. Hata hivyo baadae kidogo Wajerumani walikuja tena  na kupigana vita na Mangi wa Arusha Lavaito/Meingeanga Ndemi  mwaka 1890-1900.

No comments:

Post a Comment