Waandishi wakifanya mazoezi vitendo
Mkuu wa Idara ya mawasiliano na habari Lilian Liundi akifundisha.
Waandishi wanaoshiriki mafunzo wakiwa katika majadiliano
WAANDISHI
wa habari wameaswa kubeba sauti za wananchi walioko pembezoni katika
kudai haki zao hasa wakati wa mchakato wa kukusanya maoni ya wananchi
kwaajili ya kuandaa katiba mpya.
Akizungumza
jana Kaimu Mkuu wa Chuo cha Mafunzo ya Jinsia kilichoko chini ya
Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) Dorothy Mbilinyi, amesema watanzanzia
masikini walioko pembezoni wanategemea kupata taarifa na kutoa taarifa
kupitia vyombo mbalimbali vya habari.
“Wananchi
wameamka wameanza kujieleza vyombo vya habari vinatakiwa kufanya kazi
yake kuwa sauti ya wanyonge, viwe mdomo kwa makundi yaliyowekwa
pembezoni, ili kuibua changamoto zilizojificha na kuyafanya makundi
haya kuwa na haki sawa na wengine,” amesema Mbilinyi
Mbilinyi
amesema kuwa vyombo vya habari vya Tanzania vimefanya kazi kubwa ya
kuibua kero za wananchi na ufisadi, ikiwepo kudai uwajibikaji katika
misingi ya demokrasia na haki za biandamu.
Aidha
amewataka waandishi wa habari kufanya kazi kwa bidii mwaka huu
kwasababu ni mwaka wenye changamoto nyingi ambazo zitahitaji weledi,
uadilifu, ukweli na uwazi.” Huu nini mwaka wa kukusanya maoni ya
katiba, mwaka wa kudai uwajibikaji kwa viongozi wasio waadilifu, na ni
mwaka wa Sensa ya idadi ya watu…” amesema Mbilinyi.
Akieleza
malengo ya mafunzo hayo ya siku tatu yaliyoanza mei 3 hadi 5, Mkuu wa
Idara ya Mawasiliano na habari, Lilian Liundi amesema kuwa mafunzo hayo
yatawasaidia waandishi wa habari kujitadhimini upya jinsi ambavyo
wanaandika habari za kijinsia.
Pamoja
na kujitadhimini waandishi wa habari watajifunza juu ya hali ya sasa
ya ujenzi wa vuguvugu la ukombozi wa wanawake kimapinduzi, kampeni ya
haki uchumi, mfumo dume na mfumo uleberali mambo leo.
Pia
watajifunza namna ya kuandika habari za kijinsia na kuchambua maoni
yanayotolewa na wananchi juu ya katiba mpya, kufanya habari za
kiuchunguzi vijijini na kuibua changamoto za wananchi.
Mafunzo
haya yanafanyika ikiwa ni siku chache baada ya TGNP kukutana na
wahariri wa vyombo vya habari jijini Dar es alaam wiki iliyopita.
No comments:
Post a Comment