Mama mgonjwa mwenye maambukizi katika mfumo wa uzazi huwa na dalili zisizo na mpaka na mara nyingi huambatana na maumivu ya ghafla ya tumbo.
Kama maumivu hayo yamesababishwa na kisonono (gonococcol infection), dalili hutokea mapema sana yaani kati ya siku tatu hadi nne na kama ni wadudu wa Chylamydia huchukua siku tano hadi saba kupata maumivu ya tumbo.
Dalili nyingine ni mgonjwa kupata homa pamoja na kichwa kuuma na kutokwa na damu nyingi wakati wa hedhi na maumivu makali wakati wa hedhi, kutokwa na uchafu mzito sehemu za siri za mwanamke na kichefuchefu na kutapika.
Dalili nyingine ni maumivu wakati wa tendo la ndoa Dyspareumia, maumivu na kutokujisikia vizuri sehemu ya kulia ya tumbo upande wa juu karibu na ini, hii hutokea kwa asilimia tano hadi kumi kutokana na maambukizi kwenye mirija ya kupitisha mayai (saipingitis). Daktari akimpima mgonjwa atagundua kuwa joto la mwili limepanda kwa nyuzi joto kati ya 38.3 hadi 38.5 na akipima tumbo kwa kutumia mkono atagundua maumivu makali chini ya kitovu kulia pamoja na kushoto pia ini linaweza kuwa limevimba na linauma akiminywa.
Mgonjwa akipimwa ukeni hugundua uchafu ambao siyo wa kawaida na mzito sana na huzunguka shingo ya kizazi na ukigusa shingo ya kizazi mgonjwa husikia maumivu makali. Vitu muhimu kwa mgonjwa kugundua kuwa ana tatizo hili la PID ni kwa mama kusikia maumivu makali chini ya kitovu na daktari akiminya tumbo, mgonjwa husikia maumivu makali.
Na daktari akigusa shingo ya kizazi joto la mwili hupanda hadi kufikia nyuzi joto 38.3 na kutokwa uchafu mzito ambao ukipelekwa maabara kupimwa atagundulika kuwa ana maambukizi ya kisonono na Clamydia hivyo basi ni bora ukaanza mpango wa kupata tiba.
No comments:
Post a Comment