JESHI
la Polisi limewataka wananchi kuendelea na utulivu kama walivyoonyesha
wakati wa upigaji kura na hatimaye kupatikana katika siku ya kumwapisha Rais Mteule Dk. John Pombe Magufuli.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam, Kamishna wa
Oparesheni na Mafunzo Jeshi la Polisi, Paul Chagonja amesema kuwa jeshi la
polisi limeridhishwa na utulivu uliokuwepo wakati wa upigaji kura, na
utulivu huo umeweza kufanya uchaguzi kwenda salama na hatimaye kukaweza
kupatikana mshindi.
Amesema hali ya amani ipo na wananchi wametakiwa kulinda hali hiyo na
ikitokea mtu analeta uchochezi waripoti kwa vyombo vya usalama ili hatua
zichukuliwe.
No comments:
Post a Comment