TTCL

EQUITY

Monday, November 2, 2015

Urusi: Nguvu kutoka nje ilisababisha ajali ya ndege


''Nguvu kutoka nje'' ndio iliyosababisha ajali ya ndege iliyoanguka katika rasi ya Sinai na kuua watu 224 wengi wao raia wa Urusi.

Kogalymavia, Kampuni inayomiliki ndege hiyo ya Urusi imesema hakuna njia nyengine ya kuelezea ajali hiyo mbaya zaidi katika miaka ya hivi punde.

Katika mkutano na wanahabari jijini Moscow, afisa mmoja mkuu wa shirika hilo Kogalymavia alipinga madai kuwa ndege hiyo ilikuwa na hitilafu au makosa ya rubani.

Mabaki ya Ndege iliyopata ajali
Watu wote 224 waliokuwa katika ndege hiyo waliaga dunia.
Kogalymavia, Kampuni inayomiliki ndege hiyo ya Urusi imesema hakuna njia nyengine ya kuelezea ajali hiyo

Aidha msemaji wa kampuni hiyo amekiri kuwa ndege hiyo ilikuwa na hitilafu kwenye bawa lake lakini wahandisi waliirekebisha kabla ya ndege hiyo kupaa kutoka Sharm el-Sheikh kuelekea St. Petersburg.

Kogalymavia ambayo ndege yake ilianguka katika rasi ya Sinai nchini Misri imekanusha kuwa hiyo ndio chanzo cha ajali hiyo mbaya.

Sasa mtaalamu wa maswala ya usalama wa ndege nchini Urusi sasa anasema kuwa kuna uwezekano lilikuwa shambulizi la kigaidi ndilo lililosababisha ajali hiyo ya ndege.

Alexander Smirnov anasema kuwa inashangaza kuwa ndege hiyo ilipoteza kasi ilhali marubani wote hawakujaribu kutafuta msaada.


Mtaalamu wa maswala ya usalama wa ndege nchini Urusi sasa anasema kuwa kuna uwezekano lilikuwa shambulizi la kigaidi

Matamshi hayo ya Smirnov yanatoekea huku uchunguzi wa vinasa sauti vya ndege hiyo ukiwa bado unaendelea.

Awali,Miili ya watu 160 waliofariki dunia katika ajali ya ndege eneo la Sinai nchini Misri iliwasili mjini St Petersburg nchini Urusi

Watu wote 224 waliokuwa katika ndege hiyo waliaga dunia.

Rais wa Misri Abdel Fattah al Sisi amewataka watu wote wawe na uvumilivu wakati uchunguzi ukiendelea.

Uchunguzi wa vinasa sauti za safari ya ndege unaendelea
Mmoja wa wachunguzi wa masuala ya safari za ndege kutoka Urusi amesema kuwa ndege ya Urusi iliyoanguka katika rasi ya Sinai nchini Misri ilivunjika ikiwa hewani.

Aleksandr Neradko amesema kwamba mabaki ya ndege hiyo yametapakaa katika rasi ya Sinai.Image copyrightEPAImage caption

Wengi wa abiria waliokuwa kwenye ndege hiyo ni raia wa Urusi.

Mchunguzi kutoka nchini Urusi amesema kwamba ni mapema mno kujua chanzo cha ajali hiyo.

Wapiganaji wa kundi la Kiislamu la Islamic State walikuwa wamedai kudungua ndege hiyo, madai ambayo yamepingwa na serikali za Urusi na Misri.

No comments:

Post a Comment