Tanzania ni moja ya nchi za ukanda wa bahari ya
Hindi ambazo zinatabiriwa kuwa huenda zikakabiliwa na uhaba wa maji
pamoja na ongezeko la bei za vyakula kutokana na athari za mabadiliko ya
hali ya hewa zinazoendelea kujitokeza na kuathiri sekta mbali.
Meneja Takwimu za Hali ya Hewa nchini ,Janet Loning`o
Hayo
yameelezwa na meneja takwimu za hali ya hewa nchini , Janet Loning`o
akizungumza katika warsha ya mafunzo juu ya takwimu za hali ya hewa kwa
nchi za bahari ya Hindi pamoja na mataifa ya Ulaya inayoendelea jijini
Arusha ,
Lining'o amesema kuwa licha ya uhaba wa maji pia mabadiliko ya hali
ya hewa yanachangia kiasi kikubwa ongezeko la joto hivyo wananchi
wanapaswa kupewa elimu juu ya kukabiliana na athari zinazotokana na
mabadiliko ya hali ya hewa.
Meneja huyo amesema kuwa wanajifunza kufanya uokoaji wa takwimu za
hali ya hewa ambazo bado hazijaingizwa kwenye mfumo wa digitali kwani ni
za miaka mingi iliyopita na zinasaidia katika kutabiri iwapo kuna
uwezekano wa kutokea kwa ukame na mafuriko katika maeneo mbalimbali
nchini.
Msaidizi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini Kenya, Peter Ambenje
Amesema kuwa uhifadhi huo wa takwimu utasaidia kuzuia upotevu wa
takwimu muhimu katika masuala ya mabadiliko ya hali ya hewa.
Mabadiliko ya hali ya hewa ni tatizo linaloikumba dunia na
kusababisha madhara mbalimbali ikiwemo ukame, ongezeko la joto na uhaba
wa maji huku nchi nyingi za Afrika zikiwa ni wahanga wakubwa wa
mabadiliko hayo, juhudi za kupanda miti na kutunza mazingira zinapaswa
kuchukuliwa haraka ili kunusuru dunia na mabadiliko ya hali ya hewa.
No comments:
Post a Comment