TTCL

EQUITY

Tuesday, November 10, 2015

RAIS WA ZAMBIA AMTANGAZA NGOWI KATIKA SHEREHE ZA UAPISHO

Rais wa Zambia, Edgar Lungu akiwa amevaa suti maalum  (Presidential suit) iliyobuniwa na Mbunifu wa mavazi wa Kimataifa kutoka Nchini Tanzania Sheria Ngowi wakati wa uapisho wake baada ya kutangazwa mshindi wa nafasi ya urais baada ya kufanyika uchaguzi.
 
Rais mpya wa Zambia, Edgar Lungu akionekana kupendeza wakati akila kiapo cha kuwa Rais Mpya wa Zambia  katika sherehe zilizofanyika viwanja vya National Heroes, mjini Lusaka-Zambia. Guy Scott, of Scottish 
 
 Rais Edgar Lungu akitia saini Hati Maalum Muda mfupi baada ya kuapishwa katika sherehe.

 
Rais mpya wa Zambia, Edgar Lungu

Mbunifu wa mavazi wa kimataifa, Sheria Ngowi ameendelea kuipeperusha bendera ya Tanzania kupitia kipaji chake cha ubunifu wa mavazi baada ya kumvalisha Rais mpya wa Zambia, Edgar Lungu katika sherehe za kuapishwa kwake.

Rais Lungu 58, aling’arisha sherehe hizo baadaya kuvaa suti rasmi (Presidential suit) rangi ya bluu, shati jeupe na tai nyekundu zilizobuniwa na Mbunifu wa mavazi wa kimataifa, Sheria Ngowi. Lungu aliambatana na mke wake, Eshter Lungu walipokuwa wanaingia viwanjani hapo huku wakisindikizwa na ulinzi mkali.
 
Akizunngumza na chombo chetu cha habari Sheria Ngowi alisema ameeleza kufurahi kupata nafasi ya kipekee ya kumvalisha Rais Lungu katika sherehe za kuapishwa kwake na kusema ni hatua kubwa katika kazi yake kama mbunifu wa mavazi wa kimataifa.

"Hii ni hatua kubwa katika kazi yangu ya ubunifu wa mavazi, namshukuru Mungu kwa kipaji alichonipa kinachoweza kunitambulisha na kunifanya niaminike hata kufikia hatua ya kuvuka mipaka ya Tanzania na kumvalisha Rais mpya wa Zambia, Mheshimiwa Edgar Lungu” alisema Ngowi.
 
Mbunifu Ngowi amesisitiza kuwa juhudi, nidhamu, bidii na kumweka Mungu mbele ndio chachu ya mafanikio katika kila utendaji wa kazi zake akiwa na malengo ya kuipeleka kazi yake katika nyanja za kimataifa hata kutambulika katika sekta ya ubunifu wa mavazi duniani kote.
 
Mbunifu huyo ameendelea kuonyesha na kudhihirisha kuwa Tanzania ni nchi yenye vipaji vinavyoweza kuiletea nchi ya Tanzania sifa na kuinua uchumi wake katika sekta mbalimbali. Hii si mara ya kwanza kwa mbunifu huyo kukata mawingu kuitangaza nchi yetu, kwani ni miongoni mwa wabunifu mashuhuri kutoka Afrika wanaopata fursa kuonyesha ubunifu wa mavazi yao katika maonyesho ya kimataifa kama vile New York Fashion Week nchini Marekani na Mercedes Benz fashion Week nchini Afrika Kusini.

Hii ni changamoto pia kwa wabunifu wa Tanzania kuziwania fursa zilizopo na pia kuongeza juhudi ili kutangaza na kupeleka kazi zao katika soko la kimataifa kama vile Sheria Ngowi alivyofungua milango. 

No comments:

Post a Comment