TTCL

EQUITY

Wednesday, November 11, 2015

Stars yapoteza 2-0 kwa U 23 ya Afrika Kusini

Timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars imepoteza mechi yake ya kirafiki ya mazoezi dhidi ya timu ya taifa ya vijana chini ya miaka 23 kwa kufungwa mabao 2-0.

Mechi hiyo iliyochezwa hapo jana jioni uwanja wa Eldorado nje kidogo ya jiji la Johanesburg na muda mwingi vijana hao wanaofundishwa na Shau Bartlet aliyewahi kuchezea Charlton Athletic ya England na Bafana Bafana walitawala zaidi kipindi cha kwanza kwa kiasi kikubwa.

Baada ya mechi hiyo, Kocha Charles Boniface Mkwasa amesema, mechi hiyo ni kwa ajili ya kuangalia makosa na kipi cha kurekebisha wachezaji wake ambao walicheza kwa tahadhari kubwa kwa hofu ya kuumia.

Baada ya mechi hiyo, Stars imemaliza rasmi kambi yake ya nchini Afrika Kusini na leo inaanza safari kurejea nyumbani kwa ajili ya maandalizi ya mwisho ya mechi dhidi ya timu ya taifa ya Algeria itakayochezwa Novemba 14 uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
Kikosi cha Stars kilichoanza:

1.   Aishi Manula
2.   Shomari Kapombe
3.   Haji Mwinyi
4.   Nadir Haroub
5.   Kelvin Yondani
6.   Jonas Mkude/Himid Mao
7.   Simon Msuva
8.   Salum Abubabary/Frank Domayo
9.   John Bocco/Elius Maguri
10.Mrisho Ngassa/Malimi Busungu
11. Farid Mussa/Salum Telela

No comments:

Post a Comment