TTCL

EQUITY

Wednesday, November 11, 2015

Kikosi cha wachezaji 24 Algeria kuwasili Alhamisi

Msafara wa timu ya Taifa ya Algeria unatarajiwa kuwasili nchini siku ya Alhamisi ukiwa na jumla ya watu 65 wakiwamo wachezaji 24 tayari kwa mchezo wa Jumamosi Novemba 14 dhidi ya wenyeji Tanzania katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.


Kocha mkuu wa timu hiyo Christian Gourcuff raia wa Ufaransa ametaja kikosi cha wachezaji 24, wakiwemo wachezaji 18 wanaocheza katika klabu za Ulaya kwa ajili ya kuikabili Tanzania.

Mchezo huu wa raundi ya pili ni wa kuwania kuingia katika hatua ya makundi ya kusaka tiketi ya kombe la dunia litakalofanyika huko nchi Urusi mwaka 2018.

Wachezaji wanaotarajiwa kuwasili Alhamisi ni walinda mlango, Doukha Izeddine (JS Kabliye), M’bolhi Rais (Antalyaspor), Asselah Malik (CR Belouizdad), walinzi Zeffane Mehdi (Rennes), Medjani Carl (Trabzonspor), Ziti Mohamed (JS Kabliye), Mesbah Eddine (Sampordia), Bensebaini Ramy (Montpeller), Belkarou Hichem (Club African), Ghoulam Faouzi (Namples), Mandi Aissa (Reims).

Viungo ni Guedioura Adlane (Watford), Boudebouz Ryad (Montpeller), Taider Saphir (Bologna), Abeid Mehdi (Panathinacos), Bentaleb Nabil (Tottenham), Ghezzal Rachid (Lyon), Melsoub Walid (Lorient), Marhez Ryad (Leicester).

Washambuliaji  Benrhama Said (Nice), Sliman Islam (Sporting Lisbon), Belfodil Ishak Beni Yas), Brahimi Yassine (FC Porto) na Bounedjah Baghdad (Etoile du Saleh)

No comments:

Post a Comment