Mjadala wa wagombea
wa urais wa Marekani katika chama cha Democratic umekamilia katika
jimbo la Iowa nchini humo huku Kinara wa chama hicho na waziri wa zamani
mambo ya nje wa Marekani bi , Hilary Clinton,akisema ni sharti dunia
ipambane na itikadi za kigaidi.
Hata hivyo mmoja wa wapinzani
wake, Seneta Bernie Sanders, amemkosoa akisema sera ya Bi Clinton huko
Iraq ndizo ziliyoijengea dunia mazingira ya kushamiri kwa makundi ya
wapiganaji kama vile Al Qaeda na IS.
Bi Clinton akizungumza huko Iowa alisema swala la ugaidi sio vita vya wamarekani pekee.
Aliwataka viongozi wa mataifa ya kiarabu kufanya kazi ya ziada kupunguza mfumo unaozalisha ugaidi zaidi.
Clinton alizitaka Uturuki na mataifa ya Ghuba kusaidia kutatua tatizo la ugaidi.
Mpinzani mwengine Martin O'Malley alipinga ushauri
wa bi Clinton akidai sharti Marekani ijitwige jukumu la kupambana na
ugaidi wala sio kufwata ushauri wa Bi Clinton.
Siku ya Ijumaa
magaidi walivamia maeneo sita mjini Paris na kuwaua takriban watu 129
watu zaidi ya mia tatu wanauguza majeraha mabaya ya risasi.
Wadadisi
wa kisiasa wanasema mashambulizi hayo ya Ufaransa bila shaka yatabadili
mwelekeo wa mjadala huo huku maswala ya usalama wa ndani ya nchi
yakipewa kipao umbele.
Mjadala huo ulianza kwa watu kukaa kimya kwa mda kuwakumbuka wahanga wa mashambulio ya huko Paris.
No comments:
Post a Comment