Rais wa Marekani
Barack Obama hatimaye amejiunga na Facebook, na ujumbe wake wa kwanza
umekuwa ni wa kuhimiza watu kuchukua hatua kukabiliana na mabadiliko ya
tabia nchi.
Ikulu ya White House
kwenye ukurasa huo wake imepakia video ya Obama akitembea katika eneo la South Lawn katika ikulu ya White House.
Hatua
yake ya kujiunga na Facebook, mtandao wa kijamii wenye zaidi ya
watumiaji bilioni moja, inaonekana kama juhudi za kiongozi huyo
kuwafikia zaidi vijana na makundi mbalimbali ya watu.
“Natumai
mtachukulia huu kuwa ukumbi ambao tunaweza kutumia kujadiliana kuhusu
masuala muhimu kuhusu taifa letu,” anasema kwenye video hiyo.
Obama
anaonekana akitembea kwenye bustani hiyo ambayo imekuwa chini yake kwa
miaka saba iliyopita, ambayo kama anavyosimulia, ina mbweha, mwewe na
vichakuro.
Lengo kuu la kisiasa hata hivyo linaonekana kuhimiza ulimwengu kuunga mkono juhudi za kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.
Obama atazuru Paris mwezi Desemba, kutafuta uungwaji
mkono wa mkataba wa kuweka vikwazo kwa mataifa kuhusu viwango vya
utoaji wa gesi zinazochangia ongezeko la joto duniani.
Kutokana na
hali kwamba Bunge la Congress linadhibitiwa na chama cha Republican,
ambacho hakijatambua hatari inayotokana na mabadiliko ya tabia nchi,
anahitaji kutafuta uungwaji mkono zaidi hata nyumbani.
White House imesema inatumai Facebook itasaidia kama ukumbi wa kubadilishana mawazo.
“Ukurasa
huu utawapa Wamarekani jukwaa la kubadilishana mawazo yao na Rais
kuhusu masuala ambayo wanayajali sana,” amesema naibu mkurugenzi wa
mkakati wa dijitali katika White House Kori Schulman.
Bw Obama
alijiunga na mtandao wa kijamii wa Twitter mwezi Mei mwaka huu.
No comments:
Post a Comment