Baada ya mama yake mzazi kuona uharaka wa uelewa wa Millard,
alimuanzisha shule akiwa mdogo sana na hatimae kumaliza elimu ya msingi
akiwa na miaka 12 tu, akamaliza form four akiwa na miaka 16 mwaka 2002,
sehemu zote hizo yeye ndio alikua mdogo kuliko wote darasani kuanzia
Patandi Primary School Tengeru, Akeri Secondary School na Mbezi beach
high school.
Wakati akisubiri majibu, Millard alijiunga na Arusha College of
Electronics na kusomea ufundi wa kutengeneza satelitte dish, tv deck na
radio masomo ambayo aliyamaliza na aliyasoma kwa sababu ilikua ni kazi
ya pili aliyoipenda, baada ya hapo mama yake mzazi alishawishiwa na
marafiki zake ili Millard arudishwe shule kuendelea na masomo ya
sekondari kitu ambacho alikikubali lakini hakikua na mapokezi mazuri kwa
Millard kwa sababu yeye alihitaji kufanya kitu kingine kwa wakati ule.
Mambo yalibadilika pale uncle wake aitwae Gabriel aliekua Marekani
aliporudi Tanzania na kumshawishi mama Millard amuache mtoto afanye kile
anachotaka na anachokipenda, hapo ndipo Millard akapata nafasi ya
kwenda kujiunga na East Africa Training Institute kusomea utangazaji na
uandishi wa habari mwaka 2004.
Baada ya mwaka mmoja Millard alijiunga na TVZ Zanzibar kwa muda wa
miezi mitano na akarejea Dar es salaam April 2005 kutafuta kazi baada ya
hali kuwa ngumu kwenye familia na kukosa pesa kwa ajili ya kujiendeleza
na masomo.
Alifanikiwa kupata kazi May 23 2005 kwenye kituo cha Wapo Radio 98.0
ambayo aliambiwa hatolipwa kwa sababu kanisa lililokua linamiliki radio
hiyo halina pesa ila kwa sababu alikua na njaa ya maisha na kazi ilibidi
aifanye kama ameajiriwa, kazi ilikua jumatatu mpaka jumamosi kuanzia
saa mbili asubuhi huku kazi yake kubwa aliyopangiwa ni kukusanya habari
za bei za bidhaa na hali ya usafi kwenye masoko Dar es salaam, pia
kwenda kitengo cha MOI Muhimbili hospitali kuchukua habari za majeruhi
na vifo vya ajali mbalimbali.
Kutokana na jitihada hizo Millard alianza kulipwa shilingi elfu tano
kwa wiki mwezi wa pili baada ya kazi hivyo akawa na mshahara wa elfu 20
kwa mwezi, mshahara ambao uliongezeka na kufikia elfu 20 kwa mwezi
kwenye mwaka wa tatu na wa mwisho akiwa Wapo Radio.
Baada ya hapo Millard alijiunga na ITV/Radio One mwaka 2008 ambako
alisikika kwenye vipindi mbalimbali lakini MILAZO 101 na habari za
michezo ITV ndio vilimpa umaarufu mpaka November 2010 alipojiunga na
Clouds FM/TV na kuanza kusikika kwenye kipindi cha AMPLIFAYA december 6
2010 na baadae kukabidhiwa CLOUDS FM Top 20 June 2013.
Mpaka sasa Millard Ayo ni mmiliki wa tuzo 4 ikiwemo ya Mtangazaji
bora 2006 kutoka Tanzania Radio Awards, Website bora 2012 kutoka Vodacom
Tanzania na African Stars, na moja ni ya heshima akiwa mwandishi pekee
kutunukiwa kutoka kwenye familia ya Marehemu mwigizaji Steven Kanumba.
Kipindi cha AMPLIFAYA pamoja na website yake ya millardayo.com ndio vilivyofanya ukubwa wa jina lake uongezeke.
Kitu ambacho watu wengi hawakifahamu, kipaji cha Millard Ayo
kilionekana kwanza na aliyekua mtangazaji wa TBC1 Joseph Msami ambae kwa
wakati huo ndio aliona uwezo wa Millard na kumshawishi boss wa Wapo
radio kutoa ruhusa ya Millard kuingizwa studio kuwa mtangazaji na sio
tena ripota.
Mtu wa pili ambae ndio alizidi kumnyanyua Millard kiutangazaji ni
Godwin Gondwe ambae alimuona Millard toka akiwa Wapo Radio, kwanza ndio
alikua mtu wa kwanza kumpa Millard dili la kurekodi tangazo la radio la
bei kubwa 2007 toka ameanza utangazaji, lilikua la laki moja na nusu za
Kitanzania na ndio ilikua pesa kubwa Millard kuwahi kulipwa kwa kazi ya
mikono yake toka azaliwe, na ni pesa kubwa kuliko hata mshahara wake kwa
mwezi wakati huo ambao ulikua shilingi elfu sitini.
Shukrani za pekee kwa Reginald Mengi, Joyce Muhavile, Julius
Nyaisanga, Deogratius Rweyunga, Abdallah Mwaipaya na Isack Gamba ambao
walikua kama wazazi/marafiki wakati Millard akiwa ITV, pamoja na kwamba
kwa sasa hayupo ITV lakini urafiki wao haujaisha na Millard amekua
balozi wao mzuri.
Watu wengine waliomfikisha Millard hapa alipo kwa kiasi kikubwa ni Gardner G Habash ambae wakati Millard akiwa Wapo Radio alimsaidia sana kumpa nafasi ya kusikilizwa Clouds FM ambako alipata kazi ya kuanza na kipindi cha gospel lakini wiki hiyohiyo ndio akaitwa ITV, Reuben Ndege nae alicheza kwenye uwanja mkubwa zaidi kumsuka Millard Ayo alipojiunga na Clouds FM na alijaribu sana kumshawishi Millard kujiunga nao wakati akiwa Radio One, kiukweli siku zote amekua msaada mkubwa wakati wote na supporter mkubwa kwa Millard.
Watu wengine waliomfikisha Millard hapa alipo kwa kiasi kikubwa ni Gardner G Habash ambae wakati Millard akiwa Wapo Radio alimsaidia sana kumpa nafasi ya kusikilizwa Clouds FM ambako alipata kazi ya kuanza na kipindi cha gospel lakini wiki hiyohiyo ndio akaitwa ITV, Reuben Ndege nae alicheza kwenye uwanja mkubwa zaidi kumsuka Millard Ayo alipojiunga na Clouds FM na alijaribu sana kumshawishi Millard kujiunga nao wakati akiwa Radio One, kiukweli siku zote amekua msaada mkubwa wakati wote na supporter mkubwa kwa Millard.
Sebastian Maganga ambae ni mkuu wa vipindi Clouds FM amekua msaada
mkubwa sana kwa Millard Ayo, mshauri na hata ndugu ambae ni msikilizaji
mzuri sana pale Millard anapozungumza nae na ndio alipendekeza Millard
kuchukuliwa Radio One wakati huo.
Ruge Mutahaba amekua boss, kaka, mshkaji na mshauri wakati wote kwa
Millard Ayo, kwa kiasi kikubwa pamoja na kwamba alitoa idhini ya Millard
kujiunga na familia aliyokua anaipenda kwa zaidi ya miaka 10, amekua ni
msaada mkubwa sana kwa Millard, kuna vitu vingi Millard alikua anasema
hawezi lakini Ruge amempa neno na kumpa nguvu kwamba anaweza na ndio
mafanikio ya Millard yameanza kuonekana hapo.
Big Boss Joseph Kusaga ambae ndio MD wa Clouds FM, nae amekua
mshkaji, boss na kaka kwa Millard Ayo, nguvu ya neno lake kwamba ‘i’am
proud of you’ pekee ndio linampa Millard Ayo nguvu kubwa ya kujituma
zaidi na kutumia saa kadhaa kuandaa vipindi vyake siku zote na kujituma
zaidi.
No comments:
Post a Comment