Spika wa Bunge la Oman Mhe.
Sheikh Khalid Bin Hilal Bin Nasir Al Maawali (kulia) akiongea na Mkuu wa
Hifadhi ya Taifa Serengeti muda mfupi baada ya kupokelewa katika Uwanja
wa Seronera alipowasili kwa mapumziko mafupi. Katikati ni Afisa
Mwandamizi wa Bunge Said Yakub.PICHA NA PASCAL SHELUTETE WA TANAPA
Msafara wa Spika wa Bunge la
Oman ukishuhudia sehemu ndogo ya msafara maarufu wa Nyumbu “ Great
Migration” katika Hifadhi ya Taifa Serengeti.
Simba akiwa amejipumzikia Hifadhi ya Serengeti na kuwa kivutio kizuri kwa msafara wa Spika wa Oman na ujumbe wake.
Spika
wa Bunge la Oman Mhe. Sheikh Khalid Bin Hilal Bin Nasir Al Maawali
(kushoto) akihojiwa na Mwanahabari juu ya kilichomvutia ambapo hakusita
kusema kuwa Serengeti ni zawadi ya Watanzania tunayopaswa kuitunza kwa
faida yetu.
Makamu Mwenyekiti wa Kamati
ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira Mhe. Abdulkarim Shah (kushoto)
ambaye alikuwa miongoni mwa msafara wa Spika wa Oman akihojiwa na
wanahabari ndani ya Hifadhi ya Serengeti.
Picha ya pamoja ya baadhi ya Wabunge wa Bunge la Oman na wenyeji wao Tanzania katika Hifadhi ya Serengeti.
No comments:
Post a Comment