Albamu ya
mwanamuziki Adele huenda ikaweka historia nchini Uingereza kwa kuwa
albamu iliouza zaidi ,ikiwa tayari imeuza zaidi ya kopi nusu milioni
katika kipindi cha siku tatu pekee.
Jumla ya mauzo ya 25 ni kopi
538,000 kufikia sasa ,huku zikiwa zimesalia siku nne za chati hiyo.Ni
Albamu mbili pekee zilizouza zaidi ya kopi 500,000 katika juma moja.
Take
that Progress iliuza kopi 519,000 katika wiki ya uzinduzi wake mnamo
mwaka 2010 na Oasis Be here Now ambayo inashikilia rekodi hiyo ikiuza
kopi 696,000 katika wiki yake ya kwanza mwaka 1997.
Wakati huohuo nchini Marekani,Adele amevunja rekodi ya kuuza kopi milion 2.3 za albamu hiyo kufikia sasa.
Mauzo
ya takwimu hizo yanathibitisha kwamba huenda rekodi inayoshikiliwa na
bendi ya Nsync iliotowa albamu yake mwaka 2000 'No Strings Attached'
iliouza kopi milioni 2.4 katika wiki yake ya kwanza ya uzinduzi
ikavunjwa.
Adele alicheza single yake Hello siku ya jumamosi.Mziki huo pekee umeuza kopi milioni 2.5 katika kipindi cha wiki nne pekee.
No comments:
Post a Comment