Mafanikio
ya Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu katika klabu ya TP Mazembe kwa
kutwaa ubingwa wa Afrika ni mafanikio kwa watanzania kwa ujumla.
Ni jambo la kujisifia kwa
Tanzania kwa wachezaji hao kwa kufanikiwa kucheza na kutwaa Ubingwa wa
Afrika na kumuwezesha Samatta kuweza kuibuka mfungaji bora.
Aidha mafanikio ya Samatta na Ulimwengu yanafungua
milango ya mafanikio kwa vijana wengine wa Tanzania wanaoibuka katika
soka, hasa wenenye ari ya mchezo wa mpira wa miguu.
Baada ya ushindi huo, klabu ya TP Mazembe itaiwakilisha Afrika katika
michuano ya klabu bingwa ya dunia itakayochezwa Desemba 10 mpaka 20
Japan.
Ushindi huo umempa nafasi kubwa Samatta ya kuweza kuibuka na tuzo ya
mchezaji bora Afrika kwa wachezaji wanaocheza ligi za ndani ambaye mpaka
sasa ameingia kwenye orodha ya wachezaji 10 wanaowania tuzo hiyo.
Mshindi wa tuzo hiyo ataamuliwa kwa kura zitakazopigwa na makocha
pamoja na wakurugenzi wa ufundi wa nchi wanachama wa shirikisho la mpira
wa miguu Afrika (CAF).
Pia shirikisho hilo limetoa orodha nyingine ya wachezaji wanaowania
tuzo ya Afrika ambayo inahusisha wachezaji wanaocheza ligi za ndani au
nje ya Afrika ambapo tuzo hiyo itakabihiwa kwa mshindi Alhamisi, 7
January 2016 Abuja, Nigeria.
Hii ni fursa ya pekee na inaendelea kuiletea Tanzania sifa kubwa, na kutufanya mashabiki wa mpira wa miguu kuamini kuwa inawezekana tukiwatia moyo na kuonesha uzalendo wa kweli panapo itajika uwepo wetu kama mashabiki wa timu yetu ya taifa (Taifa Stars) na kwa wachezaji wetu popote wawapo.
Mungu ibariki Africa, Mungu ibariki Tanzania.
No comments:
Post a Comment