BENK ya Equity imeweza kupata faida ya Sh bilioni 5.03 katika kipindi
cha mwaka unaoishia Septemba 2015 ikilinganishwa na kiasi cha Sh
bilioni 1.52 zilizopatikana mwaka uliopita.
Kwa upande wa kampuni tanzu ya Equity imeweza kupata faida ya Sh
bilioni 256 katika kipindi kinachoishia mwezi Septemba 2015 ikiwa ni
ongezeko kubwa ikilinganishwa na Sh bilioni 224 iliyopatikana mwaka
jana.
Akizungumza na wanahisa kuhusu taarifa ya hesabu za robo ya tatu ya
mwaka, Ofisa Mtendaji wa kampuni tanzu ya Equity Dk James Mwangi
aliwaambia mkakati ya uboreshaji hii imewezesha Huduma za kibenki kwenye
kanda kukua kwa kasi kubwa.
Alisema pia uwekezaji mkubwa katika njia mpya za uwakala na huduma ya
simu mtandao, mafanikio yaliyopatikana katika upanuzi katika nchi za
ukanda wa Afrika Mashariki imechangia kwa kiasi kikubwa faida
iliyopatikana katika robo ya tatu ya mwaka huu.
Pia faida kabla ya kodi imeongezeka kwa asilimia 14 hadi kufikia
kiasi cha Sh bilioni 362 ikilinganishwa na Sh bilioni 318 iliyopatikana
katika kipindi cha mwaka jana.
Mafanikio haya makubwa ambayo kampuni tanzu ya Equity imeyapata
yametokana na mikakati mahsusi na ubunifu katika kuweka mazingira rahisi
ya upatikanaji wa Huduma za kibenki na kuwafanya wateja kupata huduma
hizo kwa urahisi na kwa wakati.
No comments:
Post a Comment