TTCL

EQUITY

Friday, October 30, 2015

Rais wa CAR atahadharisha kuhusu uchaguzi

Panza

Kaimu Rais wa Jamhuri ya Afrika ya Kati, Catherine Samba-Panza, ameonya kuwa maadui wa amani wanajaribu kuzuia uchaguzi mkuu nchini humo usifanyike mwezi Desemba.
Uchaguzi huo ulikuwa umepangiwa kufanyika mwezi Septemba lakini ukaahirishwa baada ya kuzuka tena kwa makabiliano kati ya Wakristo na Waislamu.
Mapigano hayo yamesababisha vifo vya watu 40.
Rais Samba Panza, amesema suluhu pekee ni kuwa na serikali halali iliyochaguliwa na raia.
“Lengo kuu la shughuli ya mpito ni kuliongoza taifa hadi kwenye uchaguzi na kurejeshwa kwa utawala wa kikatiba kwa kuwa hiyo ndiyo njia pekee,” amesema.
“Kupitia uchaguzi, raia wataweza kuchagua serikali halali ambayo itaongoza taifa hili. Hakuna njia mbadala kwetu kwa sababu hatuwezi tukakaa katika kipindi cha mpito milele.”
Rais huyo amesema hayo muda mfupi baada ya kufanyia mabadiliko baraza lake la mawaziri.
Kwenye mabadiliko hayo, Mkuu wa Shirika la Haki za Kibinadamu Afrika ya Kati Joseph
Bindoumi, anachukua nafasi ya Marie-Noelle Koyara kama waziri wa ulinzi.
Chrysostome Sambia, jenerali katika polisi, atakuwa waziri wa usalama wa umma, naye Dominique Said Paguindji, aliyeshikilia wadhifa huo awali, sasa atakuwa waziri wa haki.
Mawaziri wa ustawi mashinani na vijana pia waliondolewa.
Makabiliano kati ya Wakristo na Waislamu yamekuwa yakiongezeka nchini humo na watu wanne waliuawa kwenye barabara za mji mkuu Bangui Alhamisi.
Papa Francis amepangiwa kuzuru Bangui mwezi ujao.

No comments:

Post a Comment